Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto, Lema, Lissu njia panda, wamvaa IGP Sirro
Habari za SiasaTangulizi

Zitto, Lema, Lissu njia panda, wamvaa IGP Sirro

Spread the love

PICHA ya gari iliyoibuliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro leo tarehe 19 Oktoba 2018 kwamba ndilo lililotumika kumteka mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji (Mo) imeibua maswali mengi. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwenye mitandao ya kijamii Watanzania wamekuwa wakihoji maswali mengi kuhusu mwonekano wa picha hiyo huku wengine wakionesha mashaka ya uhusiano wa picha hiyo na kutekwa kwa Mo.

Kwenye taarifa yake na wanahabari leo jijini Dar es Salaam IGP Sirro alisema kuwa, gari hilo lililokuwa na usajili wa nje ndio lililotumika kumteka mfanyabiashara huyo.

Wakati akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, IGP Sirro alionesha picha kadhaa za gari hilo aina ya Toyota Surf yenye namba za usajili AGX 404 MC.

Mwonekano wa picha hiyo ikiwa ni pamoja mazingira lilipoegesha gari hilo, rangi yake, namna kamera za CCTV vinavyochukua picha za matukio ni miongoni mwa mambo yanayojadiliwa kwa sasa kuhusu picha hiyo ikiwemo usiri wa nchi linapotoka gari hilo.

Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa “Moyo wangu unavuja damu. IGP hapa ni collesium hotel kweli ?  IGP kwa hiyo kwenye mifumo ya CCTV baada ya kurekodi huwa kuna majira ya hali ya hewa?

“Kama hatuoneshi kuchukizwa wakati wenzetu wanapitia mateso/mauaji. Ni katika shida gani ambazo zikiwapata wenzetu tutaonyesha kuchukizwa? katika jambo hili la Mo Dewji kukaa kimya sio busara ni upumbavu mkubwa.”

Naye Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “Nimejizuia sana. Acha niseme, maana nisiposema nitaumwa. Kamanda Sirro anajua alipo @moodewji.

“IGP na Polisi wanataja njia ambayo gari ya watekaji imepita mpaka Kawe, CCTV zilikuwa zinafuata gari ile? Polisi wanaitesa sana familia ya MO na Watanzania. #SirroRudishaMO.”

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji amehoji kuhusu taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii kwa kuandika.

Anaandika Tundu Lissu

Maswali yangu kwa IGP Sirro ni haya hapa:

  1. Kama unaomba msaada wa raia wema wakupatie taarifa, halafu hutaki kutaja ‘nchi jirani’ ilikotoka hiyo gari utasaidiwaje??? Tanzania ina ‘nchi jirani’ saba, ukiachia Bahari ya Hindi. Ni ipi kati ya hizo nchi saba gari hiyo imetokea, ili usiletewe taarifa za ‘matango pori’ kutoka nchi jirani zisizohusika???
  2. Kwa nini Jeshi la Polisi la Tanzania linaamini kwamba kuomba msaada wa kitaalamu kutoka nje ni kujishushia heshima??? Kama ni hivyo, kwa nini tumetunga  Sheria ya Kusaidiana Katika Masuala ya Kijinai??? Kama tunajitosheleza katika masuala kwa nini bado tunapeleka polisi wetu nchi za nje kama Marekani kujifunza??? Au pengine sasa tumeacha kufanya hivyo???
  3. IGP Sirro anadai kama kuja hata ya kuomba msaada kutoka nje watamweleza Rais na Amiri Jeshi Mkuu atoe ruhusa hiyo. Je, hiyo ni sahihi kiasi gani wakati Sheria ya Kusaidiana Katika Masuala ya Kijinai inamtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndio aombe msaada huo???
  4. Kama wanamjua mwenye gari na dereva aliyekuwa anaiendesha kwa nini hajatoa jina au picha hadharani ili raia wema waweze kutoa taarifa wakimwona???
  5. Kuhusu motive ya kumteka Mo, polisi wana theory gani ya utekaji huo???
  6. Kuhusu wengine waliotekwa au kupotea, e.g. Ben Saanane, Azori Gwanda na Simon Kanguye, je, Jeshi la Polisi lina taarifa gani za kiupelelezi kwamba hawa wameenda ‘kutafuta maisha’ nje ya nchi na sio kwamba wamepotezwa??? Je, kuna documents zozote walizoacha kwenye exit points za mipakani, airports or seaports zinazoonyesha walitoka nje ya Tanzania???

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!