Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto kukabidhi kwa Kinana uenyekiti TCD
Habari za Siasa

Zitto kukabidhi kwa Kinana uenyekiti TCD

Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana, anatarajiwa kupokea kijiti cha uongozi wa kituo cha demokrasia Tanzania (TCD). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 5 Aprili 2022 na Mwenyekiti wa sasa wa TCD, Zitto Kabwe, wakati wa hotuba yake kwenye mkutano wa kitaifa wa maridhiano, haki na amani ulioandaliwa na kituo hicho.

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo amesema atakabidhi uongozi huo kwa chama cha mapinduzi kesho Jumatano tarehe 6 Aprili 2022, baada ya muda wake kumalizika tangu Februari mwaka huu.

Amesema aliendelea kuongoza TCD hadi sasa kutokana na kuahirishwa mara kwa mara kwa mkutano wake hivyo wajumbe wengine wakamtaka kukamilisha kwanza mkutano huo kabla ya kuondoka.

TCD ni taasisi isiyo ya kiserikali inaundwa na vyama vya siasa nchini vyenye uwakilishi bungeni, baraza la wawakili na kwenye mabaraza ya madiwani.

Vyama vinavyounda TCD kwa sasa ni pamoja na CCM, ACT-Wazalendo, Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na NCCR-Mageuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!