December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto kufuata nyayo za Tundu Lissu

Zitto Kabwe na Tundu Lissu

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amefuata nyayo za Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kufanya ziara nchini Ujerumani. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

Zitto ambaye yuko nchini Ujerumani, leo tarehe 21 Februari 2019 atafanya mazungumzo na asasi za kiraia mjini Berlin nchini Ujerumani, kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea Afrika hususan Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na John Mbozu, Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ACT, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, atahudhuria Mkutano Mkuu wa chama cha Die Linke utakaoanza tarehe 22 hadi 24 Februari 2019 mjini Bonn, Ujerumani.

“Kabla ya Mkutano huo, Ndugu Zitto atafanya mazungumzo na asasi za kiraia leo mjini Berlin, kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea Afrika hususani Tanzania,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Mbozu.

Aidha, Zitto anatarajia kufanya mazungumzo na Rais wa European Left, Gregor Gysi. Baada ya  hapo atakutana na Mbunge wa Die Linke katika Bunge la Ujerumani, Eva Maria Schreiber ambaye ni mjumbe mwenza katika programu ya “Mbunge amlinde Mbunge”.

Katika ziara hiyo, Zitto ameambatana na Mbozu, Katibu wa Ngome ya wanawake ACT, Mwanaisha Mndeme.

Kabla ya Zitto kufanya ziara hiyo, hivi karibuni Lissu alifanya ziara nchini humo kwa muda wa siku mbili na kuzungumza na baadhi ya maofisa wa serikali na wabunge wa Bunge ka Ujerumani.

error: Content is protected !!