Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto Kabwe kufichua kesi mpya za Serikali bungeni
Habari za Siasa

Zitto Kabwe kufichua kesi mpya za Serikali bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amewasilisha swali la maandishi bungeni akiitaka serikali iueleze umma kuhusu idadi ya kesi zilizofunguliwa kwenye mahakama za kimataifa dhidi yake. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Zitto ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo ameandika kuwa swali hilo la maandishi ameliwasilisha bungeni leo tarehe 4 Septemba 2018.

“Muda mfupi uliopita nimewasilisha swali la maandishi Bungeni kuitaka Serikali iueleze umma Kuhusu kesi zote ambazo Jamhuri ya Muungano imefunguliwa kwenye mahakama za kimataifa za usuluhishi ya migogoro ya Biashara, uwekezaji na mikataba. Watanzania wanafichwa Mambo mengi muhimu,” ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter.

Zitto ameandika kuwa, amechukua uamuzi huo baada ya kupitia nyaraka za kesi ya Acacia Mining dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kugundua kuwa kuna taarifa zinazofichwa kwa umma.

“Nimechukua uamuzi huu baada ya kupitia nyaraka nyeti za kesi ya Acacia Mining dhidi ya Jamhuri ya Muungano ( LCIA Arbitration No. UN173686 no. 87 ) iliyopo London na kugundua kuwa Serikali yetu inaficha Taarifa Kwa umma wakati Watanzania Ndio watalipa matrilioni ya shilingi,” ameandika Zitto.

Zitto ameendelea kuandika kuwa: “Kesi iliyoamuliwa juzi dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ilizungumzwa kwenye Taarifa ya CAG ya mwaka huu kwa Hesabu za 2016/17. Lakini pia kesi hii haikuwa yetu kwani Benki ya SCBHK haijawahi kuwa na mkataba na nchi yetu. Uzembe mkubwa umefanyika na hivyo kubambikwa kesi si yetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!