Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto Kabwe anusurika kwenda jela, ‘afungwa mdomo’
Habari za SiasaTangulizi

Zitto Kabwe anusurika kwenda jela, ‘afungwa mdomo’

Spread the love

MBUNGE wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, nchini Tanzania, Zitto Kabwe, amenusurika kifugo cha mwaka mmoja gerezani. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Huruma Shaidi, ameaimbia mahakama hiyo leo Ijumaa, tarehe 29 Mei 2020, kuwa “maneno aliyotamka Zitto hayana ukweli, makali na magumu mno.”

Amesema, “maneno yale yalikuwa strong (mazito), kwamba watu 100 kufa sio kitu kidogo. Maneno haya yameshindwa kuthibitishwa hata kwenye utetezi wake mahakamani.”

Zitto alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, tarehe 2 Novemba 2018, ambako alituhumiwa kwa makosa ya uchochezi dhidi ya jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa waendesha mashitaka wa serikali, Zitto aliitisha mkutano na waandishi wa habari, tarehe 28 Oktoba 2018, makao makuu ya ACT Wazalendo,  akiwa na lengo la kuleta chuki kwa raia wa Jamhuri, kinyume na sheria.

Katika shauri hilo, namba 327/2018, Hakimu Shaidi amesema, “haiwezi kuwa rahisi kutaja watu wa kabila fulani, kwamba wameuwa. Huko ni sawa na kuwasha moto kwenye nyasi kavu…”

“Naona huko mitandaoni kuna watu wanadai Mahakama ya Kisutu imegeuka kuwa TRA kwa sababu ya faini tunazotoa kwa watuhumiwa.

“Sasa Zitto mimi nakupa mtoto wa kulea. Sikupigi faini ila nataka usitoe kauli yoyote ya uchochezi katika Kipindi cha mwaka mmoja kutoka leo.

“Mawakili wako watakwambia nini maana ya hukumu hii. Kwa hiyo nakupa wajibu wa kulea amani ya Tanzania kwa kutotoa kauli za kichochezi.”

Amesema, maneno hayo ambayo mwanasiasa huyo aliyatamka, ni maneno ambayo hayana ushahidi wa kutosha.

Amesema, “hakuna palipothibitishwa kwamba askari wamemuua nani ana ushahidi unaonesha kuwa tukio hilo, lilifanyika alfajiri muda ambao hauwezi kusema nani alimuua nani.”

Katika uamuzi wake, Hakimu Shaidi amesema, baada ya Mahakama kumtia hatiani mwanasiasa huyo, anamuamuru  kutoandika wala kutamka maneno ya uchochezi kwa muda wa mwaka mmoja.

“Ieleweke kuwa sisi sote Watanzania. …tumlee mama yetu amani hata ninyi wanasiasa mnawajibu mkubwa  wa kumtunza,” ameeleza Hakimu Shahidi katika maamuzi yake.

Ameongeza, “mmezoea kusema kwenye mitandao kuwa Mahakama ya Kisutu imegeuka TRA (Mamlaka ya Mapato ya taifa).”

Amesema, jamii ina watu wenye uelewa na uwezo tofauti wa kuchuja maneno, hivyo kila mmoja anaweza kuchuja maneno, kwa kadri anavyoweza.

Kauli ya Hakimu Shahidi kuwa mahakama ya Kisutu imekuwa mkusanyaji mkuu wa kodi za serikali, kunatokana na matukio ya hivi karibuni, ambapo mahakama hiyo, imekuwa ikitoza faini kubwa baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara na mwandishi wa habari nchini Tanzaniai, Erick Kabendera.

Miongoni mwa watuhumiwa waliotozwa faini ya mamilioni ya shilingi, ni pamoja na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho, ambao kwa pamoja walilipishwa kiasi cha Sh. 350 milioni.

Naye Kabendera alilipishwa takribani Sh. 100 milioni, baada ya kumtia hatiani kwa makossa mawili ya “kushindwa kulipa kodi na kutakatisha fedha.”

Hakimu Shaidi alimaliza kusoma hukumu yake kwa maelezo kuwa ikiwa kuna upande haujaridhika na maamuzi yake, hiyo milango ya kukata rufaa ipo wazi.

Katika shauri hilo, Zitto alikuwa akitetewa na mawakili watatu – Jebra Kambole, Frank Mwakibolwa na Bonifacia Mapunda – huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na Tumaini Kweka na Nassoro Katuga.

Mwakibolwa ameiomba mahakama kuwa anaomba mteja wake, kupewa nafuu ya adhabu kwa kuwa baba wa watoto wadogo wanne na kwamba hana rekodi za jinai kwenye mahakama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

error: Content is protected !!