March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto Kabwe akubali yaishe matokeo udiwani

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT na mbunge wa Kigoma Mjini

Spread the love

BAADA ya kukamilika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 nchini, Kiongozi wa ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama chake kimekubali kushindwa, anaandika Hamis Mguta.

Katika taarifa aliyoitoa leo, Novemba 27, 2017 Zitto amesema ACT Wazalendo katika uchaguzi wa jana Jumapili Novemba 26, 2017 ilisimamisha wagombea katika kata 17.

“Tumepata matokeo ya kata zote na hakuna kata tuliyoshinda. Wapiga kura wameamua na sisi tumekubali. Tunafanya tathmini ya matokeo nchi nzima na tutazungumza na wananchi. Tunawashukuru kwa kura tulizopata. Tutazienzi kwa kuwa ndiyo haki yetu,” amesema Zitto.

Amesema wanajiandaa kwa uchaguzi mdogo ujao ukiwemo wa ubunge kwenye majimbo yaliyo wazi.
Zitto amesema watatumia mafunzo waliyopata kwenye uchaguzi mdogo  kujipanga kwa uchaguzi ujao.

“Kwetu sisi chama cha ACT Wazalendo, uchaguzi ulikuwa fursa ya kuzungumza na wananchi na kufikisha ujumbe wetu kwa kuwa kuzuiwa mikutano ya hadhara kunatunyima fursa hiyo. Hatutachoka kuendelea kusambaza sera zetu kwa kuwa tunaamini ni bora zaidi na zinazoweza kuleta unafuu kwa wananchi wetu,” amesema.

error: Content is protected !!