Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto Kabwe aivuruga tena serikali
Habari za SiasaTangulizi

Zitto Kabwe aivuruga tena serikali

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo. Picha ndogo Rais John Magufuli
Spread the love

KIONGOZI wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameituhumu serikali kupika takwimu juu ya kupanda kwa pato la taifa, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama chake jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Zitto amesema, “takwimu zinazotolewa na serikali juu ya ongezeko la pato la taifa ni za kupikwa.”

Amesema, ‘’…leo hii, kwa masikitiko makubwa, naomba nikiarifu kikao hiki kuwa shaka iliyokuwepo juu ya kupikwa kwa takwimu za ukuaji wa pato la taifa imekamilika. Tunaushahidi kuwa serikali inapika takwimu zake juu ya kuongezeka kwa pato la taifa na jambo hili tunaweza kulithibitisha kwa kuwa tunaushahidi usio na mashaka.’’

Zitto amerejea alichokieleza kwenye mkutano wa Kamati Kuu (CC) ya ACT-Wazalendo, kilichofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.

Kuibuka kwa taarifa kuwa serikali imepika takwimu za uchumi wake, kumekuja wiki moja baada ya Benki Kuu ya taifa (BoT), kutoa takwimu za robo ya pili ya mwaka iliyoanza Aprili hadi Juni mwaka huu.

Ukuaji wa uchumi (GDP), inachambuliwa kwa kuangalia mapato ya wananchi katika mataifa husika, ikiwamo kuondoa umasikini kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 10 kwa miaka mitano mfululizo.

Katika ripoti hiyo, serikali imedai kuwa pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 5.7; uchumi wa taifa unakuwa kwa kasi kulinganisha na mataifa mengine Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Imesema, kukua kwa uchumi kunapimwa kwa kuangalia shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo uzalishaji wa chakula na mazao, ikiwamo kilimo, mifugo na uvuvi; uzalishaji wa bidhaa za viwandani na migodini, ujenzi wa miundombinu na utoaji wa hudumaa kwa jamii ikiwemo afya, elimu na maji.

Kwa mujibu wa BoT, kiashiria kingine ni mfumuko wa bei ambao unapima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya.

Katika eneo hili, serikali inasema, mfumuko wa bei ulipungua kutoka asilimia 6.5 Januari 2016 hadi asilimia 5.5 Juni.

Akijibu madai ya serekali ya kukua uchumi, Zitto amesema, “kilichoripotiwa kwa robo ya pili ya mwaka huu na BoT ni kwamba takwimu za ukuaji wa pato la taifa ni asilimia 5.7 na mfumuko wa bei ni asilimia sita ikiwa ujazo wa fedha (M3) ilikuwa asilimia 6.1 .

“Hapa utaona ujazo wa fedha umeshuka kwa asilimia 51.5 kutoka asilimia 12.6 ukichambua utaona Tanzania uchumi wake umedumaa kwa asilimia 5.6,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa Zitto, utafiti uliofanywa na chama chake umepitiwa na wataalamu wa uchumi kutoka chama rafiki cha Lebour Party cha Uingereza na kuthibitisha kuwa takwimu za serikali zimekosewa.

Amesema, “kila mmoja sasa ataweza kujua kuwa takwimu za pato la taifa katika robo inayoishia Juni mwaka huu, siyo sahihi. Takwimu hizi zimepikwa ili kuonyesha hali ya uchumi ni nzuri, wakati ukweli ni kuwa uchumi wetu unadidimia.”

Zitto anasema, kuporomoka kwa uchumi wa taifa kunatokana na serikali kuminya sekta binafsi za fedha na hasa mikopo kwa sekta binafsi.

Akijibu swali iwapo mapato ya serikali ya kikodi kama yanaweza kubaki kama yalivyo katika kipindi ambacho mabenki na taasisi binafsi zimezorota, Zitto alisema, “haiwezekani.”

Anasema, “takwimu za makusanyo ya kodi za serikali kutoka TRA (mamkala ya mapato ya taifa) zinaacha mashaka makubwa mno kiasi cha mwenye utaalamu wa uchumi kuamini kuwa ni takwimu za kutengeneza.”

Zitto anatoa mfano wa maneno ya serikali bungeni katika mwaka wa fedha unaoishia Junia 2017 kuwa theluthi ya makusanyo ya kodi yalipaswa kutoka kwenye ushuru wa forodha.

Hata hivyo, Zitto ambaye kitaaluma ni mchumi anasema, “katika mwaka ulioshia Mei 2017, thamani ya mizigo iliyoingizwa nchini ilishuka kwa asilimia saba. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya BoT ya Juni mwaka huu.”

Zitto anasema, kuzorota kwa uchumi wa taifa kunatokana na sera mbaya za uendeshaji wa serikali ya Rais John Magufuli, ambapo amesababisha mapato ya serikali kushuka kwa kiwango cha kutisha. Hakukitaja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!