October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto hakijaeleweka kortini

Spread the love

HURUMA Shahidi, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam, ameahirisha kesi namba 327/2018, inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama ch ACT-Wazalendo, kutokana na shahidi wa Jamhuri kutohudhuria mahakamani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 29 Novemba 2019, Wakili wa Serikali Mwanandamizi, Nassoro Katuga na Wakili wa Mkuu Serikali, Tumaini Kweka wameieleza mahakama hiyo, kuwa shahidi wao anumwa.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, anatuhumiwa kufanya uchochezi alipozungumza na waandishi wa habari tarehe 18 Desemba 2018, Makao Makuu ya chama hicho Kijitonyama, jijini Dar es Salaam kuhusu mauaji yaliyotokea Uvinza, Kigoma

Hakimu Shaidi ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 3 Desemba 2019.

error: Content is protected !!