Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Zitto, Fatma Karume wazungumzia ushindi wa Dk. Hoseah TLS
Habari MchanganyikoTangulizi

Zitto, Fatma Karume wazungumzia ushindi wa Dk. Hoseah TLS

Dk. Edward Hoseah, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amemshauri Rais Mteule wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Dk. Edward Hoseah, kuwaunganisha mawakili wa chama hicho katika kutetea utawala wa sheria nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Arusha … (endelea).

Zitto ametoa ushuri huo Ijumaa tarehe 16 Aprili 2021, kupitia ukurasa wake wa Twitter, saa kadhaa kupita baada ya Dk. Hoseah kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais wa TLS katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho.

Kwenye uchaguzi huo, uliofanyika leo Ijumaa katika viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha, Dk. Hoseah alichuana na Flaviana Charles, Shehzada Walli, Albert Msando na Francis Stolla.

“Natoa pongezi zangu kwa Mwanasheria Edward Hoseah, kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa TLS na kwa wanachma wote wa TLS kwa kumaliza uchaguzi salama.”

“Tunataraji Dk. Hoseah atajitahidi kuwaunganisha wanasheria wote katika kutetea utawala wa sheria,” amesema Zitto

Naye Rais Mstaafu wa TLS, Wakili Fatma Karume, amesema, uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki, huku akimpongeza Dk. Hoseah kwa kuchaguliwa kuwa rais wa chama hicho kwa mwaka 2021/2022.

“Ni uchaguzi pekee ulio huru na wa haki Tanzania. Rais wa TLS 2021-2022 ni Dk. Hoseah. Pongezi kwake,” ameandika Fatma katika ukurasa wake wa Twitter.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TLS, Charles Rwechungura, Dk. Hoseah ameshinda kiti hicho baada ya kupata kura 293 kati ya 802 zilizopigwa.

Aliyeshika nafasi ya pili ni Flaviana, aliyepata kura 223, huku wa tatu akiwa Walli (192), wakati Msando akishika nafasi ya nne (69). Stolla alifunga dimba kwa kupata kura 17.

Kesho Jumamosi tarehe 17 Aprili 2021, Dk. Hoseah ataapishwa kuchukua mikoba ya Dk. Rugemeleza Nshala, aliyemaliza muda wake wa uongozi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

Habari Mchanganyiko

Bodi ya Maji Wami Ruvu kuchimba visima 10 kupunguza uhaba maji mikoa mitatu

Spread the love  BODI ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imesema...

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!