August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto: Bila kilimo hakuna viwanda

Spread the love

WAKATI taifa likiadhimisha siku ya maonyesho ya wakulima ya Nane nane, serikali inalaumiwa kwa kutochukua hatua stahiki katika kuboresha hali ya kilimo kwa wakulima wadogo, anaandika Pendo Omary.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo leo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema, bila serikali kuongeza uzalishaji wa tija kwenye kilimo sekta ya viwanda haitakuwa na maana yeyote.

Licha ya wakulima wadogo wadogo kuongoza kwa kukuza pato la taifa kupitia sekta hiyo, lakini bado hali ya upatikanaji wa pembejeo na masoko zimekuwa ni changamoto kuu.

“Sekta ya kilimo inapaswa kuwa sekta kiongozi katika mapambano dhidi ya umasikini na kwa kuanzia viwanda vya bidhaa za kilimo kuwa ni kiungo muhimu.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 kilimo kilikua kwa kasi ya asilimia 3.3 tu ilhali sekta hii inapaswa kukua kwa wastani wa kati ya asilimia 8 – 10 kwa muongo mmoja ili kuwezesha Nchi kutokomeza umasikini,” amesema Zitto.

Mariamu Rajabu mkazi wa Morogoro na mkulima ameiambia MwanaHALISIOnline kuwa miongoni mwa vikwazo vikubwa katika sekta ya kilimo ni serikali kuwazuia wakulima kuuza mazao nje ya nchi.

“Serikali imetuambia tujitafutie pembejeo, kwakuwa haina fedha wakati huo huo tunawekeza nguvu, muda na rasilimali zetu kwenye kulimo lakini serikali inatuzuia kuuza bidhaa zetu nje wakati ndani hakuna soko la uhakika,” ameeleza.

error: Content is protected !!