Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto azungumzia kumbukumbu ya miaka 2, kushambuliwa Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Zitto azungumzia kumbukumbu ya miaka 2, kushambuliwa Lissu

Tundu Lissu akiwa Zitto Kabwe
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amezungumzia miaka miwili tangu Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki ashambuliwe na risasi jijini Dodoma na watu wasiojulikana. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tarehe 7 Septemba 2019 akiwa nyumbani kwake jijini Dodoma.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Zitto amesema mapito anayopitia Lissu tangu kushambuliwa kwake hakuna mtu anayetamani kupitia.

“Leo imetimia miaka 2 tangu shambulizi lililokusudia kumwua Mbunge mwenzetu  Lissu. Tunamshukuru sana Mungu kwa uwezo wake na maajabu yake ambayo yamemweka hai mwenzetu na sasa amepona na kuweza kushiriki nasi katika mapambano ya kuhami na kukomaza demokrasia yetu,” ameandika Zitto.

Zitto ameshangazwa na kitendo cha vyombo vya dola vyenye mamlaka ya uchunguzi kutochunguza tukio hilo au kukamata mtu yeyote aliyehusika nalo.

“Haijapata kutokea pia tukio kama hilo kutochunguzwa na vyombo vya dola vyenye mamlaka ya uchunguzi. Miaka 2 sio tu hajakamatwa hata panzi, bali pia Lissu alinyimwa matibabu, kazushiwa kila aina ya propaganda na sasa kavuliwa ubunge, ukatili ambao haumithiliki,” ameandika Zitto.

Aidha, Zitto amezungumzia mahusiano yake na Lissu huku akieleza kwamba hawakuwahi kuwa maadui bali hawakuwa na mwono mmoja wa kisiasa.

Zitto amesema kwa sasa wamegundua kwamba tofauti zao hazikuwa na msingi wowote na kuamua kufanya kazi kwa pamoja.

“Mimi na Lissu tumeamua kwa dhati kufanya kazi pamoja kwa kuweka maslahi ya nchi yetu mbele. Wanaoturudisha nyuma wakidhani watazuia umoja huu wanajisumbua. Nchi yetu ni kubwa zaidi ya zilizokuwa tofauti zetu. Kuhami na kukomaza demokrasia yetu ni kazi ya utukufu na tutaifanya,” ameandika Zitto na kuongeza;

“Kuna watu hupenda kurudisha nyakati na kuonyesha kuwa Mimi na Lissu tulikuwa maadui. Hatukuwa maadui Lakini pia hatukuwa na mwono mmoja kisiasa. Sote tumegundua tofauti zetu hazikuwa na msingi wowote na waliotufitini kama Dk. Slaa sasa ni mabalozi wa utawala Katili.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!