March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto awataka mawaziri wa JPM wajiuzulu, kisa MV Nyerere

Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo

Spread the love

Anaandika Zitto Kabwe

Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?

Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40….. hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe. Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu.

Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ).

Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!

Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe…..Miaka 57 baada ya uhuru…Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika.

Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.

error: Content is protected !!