Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto atoa sharti kumuunga mkono Rais Samia
Habari za Siasa

Zitto atoa sharti kumuunga mkono Rais Samia

Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema, yuko tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, endapo serikali yake itahakikisha vyama vya siasa na vyombo vya habari, vitakuwa huru kutekeleza majukumu yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mwanasiasa huyo ametoa sharti hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, jana Jumanne tarehe 23 Machi 2021, wakati anazungumzia picha rasmi ya Rais Samia, iliyotolewa na Serikali.

Rais Samia amechukua madaraka kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, kwenye Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

Akizungumzia utawala wa Rais Samia, Zitto amesema yuko tayari kumpa ushirikiano wake, endapo masharti yake hayo yatafanyiwa kazi.

Pia, amesema kiu yake katika serikali hiyo, ni kuona demokrasia inatamalaki kwa kuwa ndiyo suluhisho la changamoto za Tanzania.

“Ninachohitaji katika nchi yetu pendwa ni demokrasia, demokrasia ni suluhisho la changamoto zetu.”

“Nitatoa msaada wangu kwa Rais endapo vyama vya siasa vitakuwa huru pamoja na kuhakikishiwa uhuru wa vyombo vya habari,” ameandika Zitto

Wito huo wa Zitto umetolewa siku kadhaa tangu Katibu Mkuu wa chama chake, Ado Shaibu kusema kwamba ACT-Wazalendo kiko tayari kushirikiana na Rais Samia.

Akizungumza katika shughuli ya kuuaga mwili wa Hayati Rais Magufuli katika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, tarehe 20 Machi 2021, Ado alisema kauli iliyotolewa na Rais Samia juu ya Watanzania kuzika tofauti zao na kusonga mbele, inaleta matumaini.

Na kwamba, anaamini mchango wa vyama vya siasa vya upinzani katika ujenzi wa nchi, utaheshimiwa kama ilivyokuwa zamani.

Rais Samia alitoa wito kwa Watanzania kushikamana na kuzika tofauti zao, tarehe 19 Machi 2021, wakati anahutubia taifa baada ya kuapishwa kushika mikoba ya Hayati Magufuli, Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Hayati Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani, baada ya kupata matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na mwili wake unatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Chato mkoani Geita, Ijumaa tarehe 26 Machi 2021.

Mwanasiasa huyo aliiongoza Tanzania katika kipindi cha miaka mitano na miezi mitano 5 Novemba 20215 hadi 17 Machi 2021.

2 Comments

  • Asante ndugu ndugu zitto lakini uwelewe kuwa mama watanzania wote wenye akili timamu wameshaungana na mama na wanao uhakika na uongozi wa mama na wapo tayari kulijenga taifa lao pasipo kuwa na shaka lakini tanzania inaelewa kuwa wapo wachache sana wasio itakia mema tanzania lakini wawelewe hakuna mafaniko kwa upande wao

  • Zitto demokrasia isiyo and mipakA duniani hakuna unakikumbuka ulifukizwa chama kwa sababu ya demokrasia unayoitaka wewe isiio and mipakA jirekebishe zitto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!