Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto atishiwa kuuwawa
Habari za SiasaTangulizi

Zitto atishiwa kuuwawa

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amedai kuwa, anatishiwa kuuwawa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Zitto amesambaza taarifa huyo kwenye mtandao wa kijamii wa Whatsapp wa ACT-Wazalendo kuwa, amefuatwa na mtu anayemtambua kuwa ni Usalama wa Taifa na kumpa vitisho ikiwemo kumuua.

Ameandika…

Leo baada ya kazi za Kamati yangu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii niliamua kwenda kusikiliza watoa maoni ya muswada wa sheria ya Vyama vya Siasa. Nilikwenda Kamati ya Bunge ya Katiba na sheria, nikakuta wanavunja kanuni za Bunge Kuhusu nani anaruhusiwa na Kamati kutoa maoni. Wabunge wa Upinzani akina Ally Saleh, Saed Kubenea, Salome Makamba na Anatropia Theonest walikuwa wanamwelewesha Mwenyekiti wa Kikao kwa ustaarabu kuwa anavunja kanuni. Nami nikasimama mara kadhaa kuhoji. Walikuwa wanazuia wabunge wa Kamati nyengine kuchangia hoja mbalimbali.

Baada ya kurushiana maneno kidogo Mkt akaagiza nitoke nje. Nilipotoka nje Afisa usalama mmoja akanifuata kwa nyuma na tulifika nje ya ukumbi tu akaanza kunitisha kuwa atanimaliza kwa nini nafanya fujo. Akaninyooshea kidole na kusema ‘ wewe dawa ni kukuua tu’!

Nilikasirika Sana.

Nikamjibu kwa kumwuliza Wewe ni nani? Akasema acha kujifanya unajua. Nikamwambia Huna mamlaka ya kumhoji Mbunge yeyote chochote. Nikamkaribia nikamwambia ‘ kawaambia hao waliokutuma kuwa kabla hamjaniua watakufa wao wapumbavu’. Nikapaza sauti kali. Akaja Mbunge David Silinde akapaza sauti ‘ wewe unataka nini? Akawa Anamfuata kwa kasi. Huyu Bwana akaanza kuondoka. Wakatoka pia maafisa wa Bunge na baadhi ya wabunge ( naamini baada ya kusikia mzozo ). Akakimbilia Chumba kingine hapo hapo ukumbi wa Msekwa pale walipokuja wabunge na maafisa wengine wa Bunge kufuatia kelele zile.

Huyu kijana wa Usalama amekuwa ‘akinifuatilia’ muda mrefu siku ya leo. Tukiwa tumekaa kantini na wabunge kadhaa wa upinzani na CCM alikuwa amekaa karibu yetu akirekodi tunayoongea. Tukaambizana huyu anafuatilia mazungumzo yetu tukampotezea. Sikumwona alipokuja kwenye kamati ukumbi wa Msekwa Lakini Silinde alimwona alipotufuata na Ndio maana alipoona ameinuka kitini na mzozo nje ya ukumbi akanifuata kwa kasi.

Nimeandika Barua ya malalamiko rasmi kwa Spika wa Bunge ili waweke on record. Nimekuwa Mbunge miaka 14 sasa na sijaona hali hii ya wabunge kukoseshwa amani na maafisa wa usalama wa Taifa. Hakika Bunge limekuwa Idara tu ya Tawi la Utendaji ( Executive).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!