July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto ataka ripoti ya CAG ifanyiwe kazi

Kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe

Spread the love

SIKU moja baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, kuwasilisha ripoti tano za ukaguzi wa fedha kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2014, ikibainisha ufisadi wa zaidi ya Sh. 600 bilioni, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, ametaka hatua zichukuliwe. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Zitto ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), amesema fedha iliyokwepwa idara ya forodha peke yake inalipa madeni yote ya wakandarasi wa barabara wanaoidai Tanrads na riba kulimbikizwa kila mwaka.

“Fedha hii ingelipa madeni yote ya mfuko wa PSPF wanayoidai Serikali. Fedha hizi zingeweza kulipia miradi miwili mikubwa nchini ya BVR na vitambulisho vya Taifa ambayo inasuasua kutokana na ukata.

Katika hoja yake ya kwanza, Zitto amesema, “taarifa nyingine ya CAG imetoka, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri na kwa mujibu wa sheria za nchi. Taarifa hii imechelewa kutolewa kulingana na mabadiliko ya ratiba za Bunge ambapo hapo awali ilikuwa ikitoka Aprili na kuwezesha kuchangia katika mchakato wa Bajeti ya nchi.”

Amesema taarifa ya mwaka huu na ile ya mwaka jana, imetoka wakati wa Bunge la Bajeti na hivyo, bajeti ya serikali haijazingatia hoja za ukaguzi ili kuboresha mfumo wa matumizi ya fedha za umma. Kwamba ni vema utaratibu wa zamani wa ripoti kutolewa Aprili urejewe ili wabunge waweze kutumia ripoti hizo wakati wa kamati katika kujadili makadirio ya bajeti za wizara mbalimbali.

Pili, Zitto anasema taarifa hiyo kama miaka iliyopita bado sio nzuri. “Mapato mengi ya serikali bado yanapotea. Ukurasa 53 wa taarifa unaonyesha kuwa mizigo inayoingizwa nchini kupita kwenda nchi jirani zinazotumia bandari zetu hubakia nchini na kuingizwa sokoni, hivyo kukwepa kodi.”

Ameongeza kuwa, mwaka 2013/2014, mizigo ya transit iliyobaki nchini kiudanganyifu ilikuwa zaidi ya bidhaa 6000 kwa mujibu wa taarifa ya CAG. Hivyo kodi ya Sh. 836 bilioni haikulipwa kwa mizigo hiyo sawa na asilimia 10 ya makusanyo yote ya kodi za ndani.

“Shilingi 836 bilioni ilipotea mwaka 2013/14 peke yake. Wakati hili linatokea serikali ipo katika ukata mkubwa na kushindwa kuendesha miradi yake mbalimbali. Natoa wito kwa CAG kwanza kuweka wazi orodha ya bidhaa hizo zilizobakia nchini na kuingizwa nchini bila kulipa kodi. Vile vile CAG aweke wazi wafanyabiashara wote walioagiza bidhaa hizi na vyombo vya kiuchunguzi vichukue hatua za kuwashtaki wafanya biashara hawa mara moja,” amesema.

Zitto ametoa wito kwa PAC kuwaita mara moja maafisa wa TRA kujieleza mbele ya kamati kuhusu suala hili na kuandaa taarifa maalumu bungeni ili kuanika uoza huu unaopoteza mapato mengi sana ya serikali.

Katika hoja ya tatu, Zitto anasema CAG kaonyesha kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana kitengo cha maafa cha ofisi ya Waziri Mkuu ambapo Sh.163 billioni za chakula cha maafa hazikukusanywa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

Anasema “huu ni kama mrija wenye wastani wa Sh. 32 bilioni kuchotwa kwa kisingizio cha chakula cha maafa kwa wananchi. Kwa malezo ya CAG ni kwamba watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekula fedha za chakula cha misaada.”

“Maana hakuna uthibitisho wa kuwa mahindi yaliyogawanywa na taarifa kutolewa na Wakala wa Akiba ya Chakula (NFRA). Kitengo cha maafa ofisi yake kimekuwa mrija wa wizi wa fedha za umma, wizi ambao umekuwa ukifanyika bila ya kugunduliwa kwa miaka 5 sasa.

Nne, anasema ACT- Wazalendo inalitaka Bunge kuchukua stahiki dhidi ya Wizara ya Ujenzi kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha kuwa wizara ilidanganya Bunge katika kupitisha bajeti ya Sh. 252 bilioni ambapo kati yake Sh.87 bilioni ziliibiwa au matumizi yake kutoeleweka.

error: Content is protected !!