Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto ataja mambo 3 mwiba kwa Taifa
Habari za Siasa

Zitto ataja mambo 3 mwiba kwa Taifa

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimesema Serikali kama haitatatua changamoto sugu zinazowakabili wananchi hususan ugumu wa maisha, migogoro ya ardhi na ukosefu wa ajira kwa vijana, nchi inaweza kupata amdhara makubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 12 Februari 2024 na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, unaofanyika jijini Dar es Salaam.

“Kuna masuala mahususi ambayo yasipochukuliwa hatua, yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa Taifa letu. Baadhi ya masuala hayo ni pamoja na; Migogoro ya ardhi na migogoro ya mipaka kati ya hifadhi na vijiji. Kupanda kwa gharama za maisha kunakopelekea kufanya wananchi kushindwa kumudu maisha ya kila siku na ukosefu ajira za vijana,” amesema Zitto.

Kuhusu migogoro ya ardhi, Zitto amedai imekithiri katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania ambapo ziara iliyofanywa na chama chake imekumbana na malalamiko kutoka kwa wakulima dhidi ya wafugaji kubamia maeneo yao na hata kupelekea mauaji.

“Vilevile maeneo ya wafugaji tumekutana na malalamiko ya wananchi kuporwa mifugo yao na maafisa wa hifadhi mbalimbali kama vile TANAPA, TFS na Mamlaka ya Ngorongoro. Migogoro ya namna hii imesambaa kila kona ya nchi yetu na isipochukuliwa hatua, italeta vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuhatarisha utulivu wa nchi yetu,” amesema Zitto.

Zitto, ameitaka Serikali kufanyia kazi suala hilo kwa kuunda tume ya Rais ya kutazama mipaka ya vijiji na hifadhi au mapori ya akiba, ili kukwepa migogoro kati ya mamlaka ya hifadhi na wananchi.

Kwa upande wa ongezeko la gharama za maisha, Zitto ameitaka Serikali kuhakikisha wananchi wanamudu maisha yao kwa kubuni, kutunga na kutekeleza sera zinazohakikisha kuwa bei za bidhaa muhimu kama chakula, mavazi na usafiri haziwi mzigo kwao.

“Ajira kwa vijana imekuwa ni changamoto ya kudumu na mwiba mchungu kwa Taifa letu kwa sababu Serikali haijielekezi kisera kujenga uchumi unaozalisha ajira nyingi, bora na zenye staha. Katika ziara yetu mikoani tumesikitishwa sana na kusuasua kwa miradi miwili mikubwa yenye faida kubwa kwa uchumi wetu na yenye fungamanisho imara kwa sekta nyingi za uchumi,” amesema Zitto.

1 Comment

  • Kuporwa ardhi, mifugo, nyumba na Mali nyinginezo inatokana na kuporomoka kwa maadili, uroho na uchoyo. Viongozi Kushindwa kusimamia maadili ya kazi nk. Kupanda kwa bei kunatokana na baadhi ya watumishi wa umma na wafanyabiashara kukosa uaminifu uadilifu na upendo kwa watanzania wenzao. Ubinafsi umekuaa mkubwa kuliko kujaliana. Watu wanataka kujilimbikizia Pesa na kamwe hazitawatosha. Suala la ajira linahusisha mambo mengi; Mosi, ni uwezo hasa uaminifu wa Wahitimu. Wahitimu wengi kama ulivyo kwa baadhi ya wenzao waliopo kazini wanauwezo na uaminifu mdogo. Maadili ndiyo changamoto kubwa ya Taifa letu. Changamoto hii inaanzia ngazi ya juu Hadi ngazi ya familia. Nayeyote atakaye jaribu kurejesha maadili lazima anatengenezewa zengwe na kupotezwa kabisa kwenye mstari. Nivigumu kumwajiri mtu asiye mwaminifu kwasababu ni hasara kubwa kwa mwekezaji. Nimeona serikali imeweka viruzu mitaala ya Elimu Somo la maadili pamoja na amali vimeingizwa kwenye mitaala ngoja tusubiri miaka ijayo tuone. Kilicho baki ni kuanzisha Somo la utawala Bora. SOMO hilo litatusaidia Sana mbeleni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!