April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto ashikiliwa Z’bar, Uhamiaji wamkabidhi kwa Polisi

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amekamatwa na Maofisa Uhamiaji Visiwani Zanzibar, akiwa njiani kuelekea nchini Kenya, kabla ya kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa ya kushikiliwa Zitto imetolewa leo tarehe 11 Juni 2019 na chama cha ACT -Wazalendo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Zitto anashikiliwa na maofisa hao tangu saa nane mchana, kwa kile kilichoelezwa kuwa haruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi.

“Chama Cha ACT Wazalendo kinajulisha wanachama wake na Watanzania kuwa Kiongozi wetu wa Chama, Zitto Kabwe ameshikiliwa na mamlaka za Serikali tangu saa nane mchana leo.

“Kiongozi ameshikiliwa na maofisa wa Uhamiaji Zanzibar kwa maelekezo kuwa haruhusiwi kusafiri kwenda Nje ya nchi. Alikuwa Akisafiri kwenda nchini Kenya,” inaeleza taarifa ya ACT-Wazalendo.

Zitto baada ya mahojiano alitolewa Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji Zanzibar na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi Ziwani.

MwanaHALISI ONLINE ilimtafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu kwa ajili ya kujua undani wa tukio hilo, ambaye amesema kwa sasa wanafuatilia kujua sababu za Zitto kuzuiwa kusafiri nje ya nchi.

Aidha, Ado amesema baada ya chama hicho kubaini sababu hizo watatoa taarifa kwa umma.

error: Content is protected !!