October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto aongeza nguvu Chadema

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalando

Spread the love

HATUA ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa kumwandiskia barua Rais John Magufuli kuhusu uchaguzi huru na haki, imepokewa kwa mikono miwili na Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, ameunga mkono hatua ya hiyo baada ya Mbowe kukutana na wanahabari jana tarehe 3 Februari 2020, na kusoma barua hiyo hadharani.

Zitto aliyeko ughaibuni kwa ziara ya kikazi, ametoa msimamo huo tarehe 3 Februari 2020 kupitia ukurasa wake wa Twitter, huku akimpongeza Mbowe kwa hatua hiyo.

“Naunga mkono barua iliyoandikwa na Chadema kwenda kwa Rais Magufuli kuhusu umuhimu wa uchaguzi huru, haki na unaoaminika. Nampongeza kwa kuongoza juhudi hizi za kuhami demokrasia yetu,” ameandika Zitto.

Wakati akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema katika barua hiyo kuna mapendekezo matatu, ambayo wameyawasilisha kwa Rais Magufuli, ili ayafanyie kazi kuelekea maandalizi ya uchaguzi huo unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba 2020.

Mapendekezo hayo ni, marekebisho madogo ya katiba na sheria mbalimbali za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa wa huru na haki.

Kurudiwa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwezi Novemba 2019 pamoja na uundwaji wa Tume ya Maridhiano ya Kitaifa.

Mbowe amesema Chadema imeamua kuchukua hatua ya kumwandikia barua Rais Magufuli, baada ya kuona taifa linapitia katika sintofahamu kubwa pamoja na hatari ya umoja wa taifa kuvunjika.

“Mhehsimiwa Rais, taifa letu linapita katika sintofahamu kubwa, kuna vaishiria vingi vinavyoashiria hatari ya  kutengwa na jamii ya kimataifa. Wakati huo huo kuna mfarakano mpana ukiendelea kuutafuna kwa kasi umoja wetu wa ndani kama taifa, hali hii haipaswi kuendelea kama ilivyo,” amesema Mbowe wakati akisoma barua hiyo mbele ya Wanahabari.

Kufuatia changamoto hizo, Mbowe amesema Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kukabiliana nazo. Hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

“Chadema kama chama kikuu cha upinzani inaamini kuna kila sababu za kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hizi. Na wewe kama rais una mamlaka yote ya kuanzisha mchakato wa kurudisha mtengamano wa nchi yetu,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Huu ni mwaka wa uchaguzi unahitaji busara uelewa na uvumilivu ili kuivusha nchi salama, kwa hali ilivyo sasa kuna kila aina ya viashiria vya uwepo wa machafuko ya kisiasa kabla, wakati na baada ya uchaguzi.”

“Kama hatutazika viburi vyetu vya kiitikadi na badala yake kusimama kama taifa, kuruhusu haki na demokrasia ya kweli kutamalaki katika kipindi chote cha mwaka huu wa uchaguzi,” alisema Mbowe.

error: Content is protected !!