Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto amwandikia barua Rais Samia, apendekeza mambo matano
Habari za SiasaTangulizi

Zitto amwandikia barua Rais Samia, apendekeza mambo matano

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amemuandikia barua, Rais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan, kumwelezea changamoto zilizojitokeza katika chaguzi ndogo za Ubunge wa Buhigwe na Muhambwe, mkoani Kigoma, ili azitafutie ufumbuzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumatano tarehe 19 Mei 2021 na Salim Biman,  Katibu wa Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT-Wazalendo, kupitia taarifa yake kwa umma juu ya tathimini ya chama hicho kuhusu chaguzi hizo zilizofanyika Jumapili iliyopita ya tarehe 16 Mei 2021.

“Zitto amemuandikia barua Rais Samia kumueleza changamoto zilizojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa.”

“Kiongozi amemueleza rais kuwa, mifano yaliyotumika katika chaguzi hizi haitoweza kutimiza nia yake njema aliyonayo juu ya kuendeleza demokrasia na kuweka mwekeleo wa shughuli za kisiasa zenye tija na maslahi kwa nchi yetu. Kama alivyoahidi katika hotuba yake bungeni alipolihutubia Taifa,” imesema taarifa ya Bimani.

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo

Bimani amesema, katika barua hiyo, Zitto amependekeza mambo matano kwa Rais Samia, yenye lengo la kuimarisha demokrasia na shughuli za kisiasa nchini pamoja na chaguzi kuwa za huru na haki.

Katika barua hiyo,  chama kimewasilisha kwa rais mapendekezo yafuatayo ili kuzifanyia chaguzi kuwa za ushindani, huru na zenye uwanja sawa wa vyama vyote vinavyoshiriki.

Pendekezo la kwanza ni uanzishwaji  mchakato wa kuifanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),  ifanye shughuli zake kwa uhuru.

“Kwamba NEC iwe na watumishi wake wanaowajibika kwa tume tu na wasiwe makada wa chama kingine cha siasa,” amesema

Pili, ni “kuanzishwa kwa mchakato shirikishi wa kupitia upya Sheria ya Vyama vya Siasa, ili kuondoa vifungu vyote vinavyobana uhuru wa vyama vya siasa kutekekeza majukumu yake. Tumetaka vyama  viwe na uhuru wa kufanya mikutano yake bila bugudha.”

Tatu, ni uanzishwaji wa majadiliano baina ya Rais Samia na vyama vya siasa, kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

“Kwa kupitia taasisi zinazomilikiwa na vyama nchini hususani  TCD, rais aanzishe majadiliano miongoni mwa vyama ili kujenga kuaminiana na kutatua migogoro kwa njia za amani pale inapotokea,” imesema taarifa ya Bimani.

TCD, inaundwa na vyama vyenye wawakilishi bungeni kwa maana ya CCM, CUF, Chadema na ACT-Wazalendo na Mwenyekiti wa kituo hicho kwa sasa ni, Zitto.

Pendekezo la nne ni “kutekelezwa kwa makubaliano ya mabadiliko ya msingi katika Katiba na Sheria ya Uchaguzi ya Septemba 2014,  kati ya Serikali na vyama kupitia TCD ili kuwezesha siasa zenye tija na chaguzi kuwa huru.”

Pendekezo la mwisho ni Rais Samia, kuvisihi vyombo vya ulinzi na usalama kufuata sheria inapovisimamia vyama hivyo.

“Pendekezo la tano ni kuvinasihi vyombo vya ulinzi na usalama, kutenda haki kwa wote na kuachia mara moja wanachama wetu na vyama vingine vya siasa, waliokamatwa na kuwekwa magerezani nyakati za chaguzi,” amesema Bimani.

2 Comments

  • Tatizo kubwa linalovikumba la vyama za siasa nchini si ukosekanaji wa demokrasia tu, bali vinahitaji kujitathimini namna vinavyojiongoza vyenyewe. Viongozi waache huruka ya kuweka maslahi yao mbele waweke maslahi ya vyama vyao mbele. Kuna vyama vingi vina migogoro ya ndani ambayo imesababishwa na kutokuwepo uwazi wa matumizi ya mapato ya vyama husika.Chama chochote cha siasa kinaweza kuwa na nguvu ya kisiasa endapo kitakuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi pia. Kwa vyama vyetu ni tofauti kwa kuwa vingi vinategemea ruzuku tu. Viongozi lazima wafiri nje ya box kuleta matokeo chanya yanayoweza kutoa ushindani zidi ya chama tawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!