Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto amuomba radhi CAG Kichere
Habari za SiasaTangulizi

Zitto amuomba radhi CAG Kichere

Spread the love

 

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amemuomba radhi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za SerikalI (CAG), Charles Kichere kufuatia hatua yake ya kupinga uteuzi wake mahakamani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Zitto ameomba radhi hiyo leo Jumapili tarehe 11 Aprili 2021, wakati akichambua Ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020, jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo kijana amesema, uamuzi wa kumpinga CAG Kichere ilisukumwa na nia yake ya kutaka misingi ya Katiba kulindwa.

“Namuomba radhi, ilikuwa hasira ya kutaka Katiba ilindwe na ameonesha kwa vitendo, kwamba anafanya kazi yake kwa weledi.

“…na nashukuru kwa taarifa yake na ameonesha amefanya kazi kwa weledi, na sasa tunajadili taarifa yenye mambo mazito,” amesema Zitto.

Akizungumzia ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma hivi karibuni, Zitto amesema ripoti hiyo imeondoa mashaka yake dhidi ya utendaji wa CAG Kichere.

“Mwanzo tulisema ameteuliwa kwenda kulinda maslahi na serikali na watu wake, yalimuumiza Kichere. Wakati ule alimtuma mbunge mwenzangu, aje kuniambia nimuamini yeye ni professional atafanya kazi yake kwa weledi nisubiri nione.

“Hakika ameni-prove wrong (amenihakikishia nilikosea) kwa ripoti yake ya mwaka huu ameonsha kwamba, hasira zangu juu yake wakati ule ilikuwa misplace (si sahihi).

Baada ya CAG Kichere kuteuliwa na Hayati Rais John Mgaufuli tarehe 3 Novemba 2019, kumrithi Prof. Mussa Assad, Zitto alitinga Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, kupinga uamuzi huo.

Akidai kwamba Prof. Assad ameondolewa kabla ya muda wake wa utumishi kukoma kwa mujibu wa Katiba.

1 Comment

  • Hongera Zitto kwa kuonesha uungwana. Ni mfano mzuri kwa wanasiasa na wakuu wote. Hakuna aibu kujikosoa na kuomba radhi. Hongera tena

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!