April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto amsaka Ongangi, ataka Kenya iingilie

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini ameitaka serikali ya Tanzania kulipa uzito suala la kutekwa kwa Raphael Ongangi, Rais wa Kenya ambaye ni msaidizi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Amesema, Ongangi ana haki ya kupatikana akiwa hai na kuungana na familia yake. Raia huyo wa Kenya, alitekwa na watu wasiojulikana tarehe 24 Juni 2019 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 1 Julai 2019 Magomeni jijini Dar es Salaam, Zitto ameiomba Serikali ya Kenya kuzungumza na serikali ya Tanzania namna ya kumpata raia wake.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, marafiki wa Ongangi wamefuatilia tukio la kutekwa kwa raia huyo wa Kenya, na kufanikiwa kupata baadhi ya taarifa muhimu.

Kama hatoachwa na watekani Zitto amesema, wako tayari kukabidhi Serikali ya Kenya ushahidi kuhusu tukio la kutekwa kwa raia wake.

Na kwamba, ni pamoja na maeneo mbalimbali ambayo amefikishwa tangu alipotekwa na watu hao.

“Naiomba Serikali ya Kenya iitake Serikali ya Tanzania kumwachia raia wao. Serikali zinajua namna ya kufanya mazungumzo baina yao.

“Sisi tunaikabidhi Kenya ushahidi kwa kila mahali alipokuwa Raphael, ili ione namna bora ya kwenda kumuokoa raia wao,” amesema Zitto.

Pia amesema, wamekabidhi sehemu ya taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi ili wachukue hatua na kwamba, kama vyombo vya usalama nchini vitashindwa kufuatilia suala hilo, waruhusu watu wa nje waje kumwokoa Ongangi.

Zitto amesema, wamefikia hatua ya kutoa wito kwa Serikali ya Kenya baada ya jitihada zake za kuzungumza na vyombo vya dola, kuhusu kuachwa huru kwa Ongangi kutofua dafu.

“Sisi marafiki wa Raphael (Ongangi) kila tunapokwenda kufuatilia tunaambiwa ataachiwa tu, tusiwe na wasiwasi. Kila tunayeongea naye serikalini na kwenye vyombo vya dola anatuambiwa kuwa tutulie ataachiwa. Siku saba zimepita sasa,” amesema Zitto.

Amesema, amefuatilia kwa mamlaka za Tanzania bila mafanikio, ikiwemo kuwaandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola pamoja na Waziri George Mkuchika ambao wote waliahidi kufuatilia suala hilo lakini hajapata jibu lolote kutoka kwa viongozi hao.

Aidha, Zitto amezitaka Jumuiya za Kimataifa kukemea vikali vitendo yanayoendelea nchini Tanzania, dhidi ya wanasiasa wa upinzani na watu wa karibu nao.

Hata hivyo Zitto ameeleza kuwa, Ongangi alitekwa akiwa Oysterbay jijini Dar es Salaam akiwa na mke wake Veronica na kwamba, gari moja liliwazuia kwa mbele na bastola kisha kuwachukua wote wawili.

Baadaye mkewe (Veronica) aliachwa huku wakitokomea na Ongangi. Wawili hao walikuwa wametoka kwenye kikao cha wazazi kwenye shule wanayosoma watoto wao.

error: Content is protected !!