Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto: Amri ya Rais Magufuli yanikamatisha
Habari za SiasaTangulizi

Zitto: Amri ya Rais Magufuli yanikamatisha

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo akizungumza na waandishi wa habari muda mchache baada ya kuachiwa kwa dhamana na polisi. Picha ndogo Rais John Magufuli
Spread the love

ZITTO Zuberi Kabwe, Kiongozi wa Chama cha Act – Wazalendo anasema alijua atakamatwa kutokana na tamko la Rais Dk. John Magufuli kutangulia kuelekeza kuwa akamatwe; na “ningeshangaa nisingetiwa mbaroni,” anaandika Faki Sosi.

Zitto amehojiwa kwa takribani saa nne tangu alipokamatwa saa moja asubuhi kutoka nyumbani kwake Mbezi Beach hadi kituo cha Polisi cha Chang’ombe yaliko makao makuu ya Mkoa wa Temeke Kipolisi.

Baadaye alipelekwa Kitengo cha Upelelezi wa uhalifu wa masuala ya uchumi na fedha kilichopo eneo la Kamata, Gerezani Dar es Salaam ambako aliachiwa kwa dhamana.

“Kila mtu alitarajia kuwa tutakamatwa maana yake Rais alisema kwamba nikamatwe… tusingekamatwa tungeshangaa kwa hiyo la ziada tusubiri mahakamani kitakuaje,” amesema Zitto.

Zitto amesema mahala pekee pa kubaini kama amefanya makosa ni mahakamani alikosema anasubiri apelekwe huko.

“Tunasubiri lini watatupeleka mahakamani ili kutetea yale tuliyoyaeleza… na mahakama ipo wazi mutaona kitachoendelea,” anasema.

Wakili wa Zitto, Steven Mwakibolwa amesema Zitto amehojiwa kutokana na hutuba ya kampeni za udiwani aliyoitoa Kijichi, jijini Dar es Salaam.

Amesema baada ya kutolewa Chang’ombe alifikishwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka (DCI) inayohusu masuala ya fedha na uchumi.

Makosa anayotarajiwa kushtakiwa nayo ni mawili; la kwanza ni kuchapisha taarifa kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mitandao na nyengine kutoa takwimu za uongo kinyume na kifungu cha 375 cha sheria ya 2015.

Amesema upelelezi wa shauri hilo unaendelea na kwamba amedhaminiwa na kutakiwa kuripoti tena Jumanne ijayo.

Awali Zitto alishikiliwa kwenye kituo cha Polisi cha Chang’ombe na kuhojiwa kuhusu hutuba aliyoitoa Jumapili kwenye kampeni za udiwani katika kata ya Kijichi aliyodaiwa kutoa maneno ya uchochezi.

Katika kampeni hizo Zitto alishutumu Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa imeshindwa kusimamia usalama wanchi na wananchi kutokana na matukio ya kushambuliwa, kuuwawa na kutekwa kwa wananchi.

Baada ya kuhojiwa aliachiwa kuachiwa  kwa dhamana kisha alikamatwa  tena na kufikishwa kwenye kitengo cha upelelezi wa masuala ya fedha na uchumi, na kuhojiwa kuhusu taarifa ya kamati kuu ya chama hicho iliyokosoa taarifa ya serikali kuhusu kupanda kwa pato la taifa kwa asilimia 5.7.

Awali tarehe 28 Oktoba, Zitto aliituhumu serikali kupika takwimu kuhusu kupanda kwa pato la taifa.

Zitto alisema taarifa ya serikali ya pato la taifa ambayo ni asilimia 5.7 imepikwa na kwamba uchambuzi ulifanywa na chama chao na wachambuzi wa nje ulibaini takwimu hizo za serikali hazina ukweli ukiowanisha na hali halisi ya uchumi wa nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!