October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto ampa ujumbe Jaji Mutungi ‘busara itumike’

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe amemshauri Msajili wa vyama vya siasa nchini humo, Jaji Francis Mutungi kutoingilia ratiba ya kongamano waliloliandaa. Anaripoti Patricia Kighono, TUDARCo … (endelea).

Zitto amesema, viongozi wakuu wa TCD ambao ni, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi, ACT-Wazalendo na Chama cha Demokraisa na Maendeleo (Chadema), wamekubaliana kufanya kongamano tarehe 21 na 22 Oktoba 2021.

Tarehe kama hizo yaani 21 Oktoba 2021, Jaji Mutungi amekwisha kutangaza kutafanyika kikao baina ya wadau wa vyama vya saisa, ofisi ya msajili na jeshi la polisi kujadili namna bora ya kuendesha shughuli za kisiasa.

Tayari vyama vinne vya upinzani vyenye nguvu, CUF, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi na Chadema vimetangaza kutoshiriki kikao hicho.

Jaji Francis Mungi, Msajili wa Vyama vya Siasa

MwanaHALISI TV na MwanaHALISI Online limefanya mahojiano maalum na Zitto kuhusu mkanganyiko huo wa tarehe na kugusia masuala mbalimbali ikiwemo kikao chake na Jaji Mutungi.

Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo amesema, hakuna kinachoshindikana, kikubwa ni busara itumike kwani kongamano kubwa la kitaifa kujadili amani, haki na maridhiano linakutanisha vyama vyote, jeshi la polisi na wadau wengine.

Amesema, kikao cha msajili kinaweza kufanyika kabla au baada ya kongamano.

Undani wa mahojiano hayo, fuatilia hapa;

error: Content is protected !!