May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto amlilia mbunge aliyefariki dunia

Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama

Spread the love

 

KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema, kifo cha mbunge wake wa Konde, Khatib Said Haji, ni pigo kwa chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Haji amefariki dunia, alfajiri ya leo Alhamisi, tarehe 20 Mei 2021, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kutokana na kifo huo, Zitto ameandika katika Twitter yake “Tumepata msiba mkubwa. Natuma salaam zangu za rambirambi kwa familia ya ndg Khatib na kwa Wananchi wa Jimbo la Konde.”

“Hakika tumepoteza mpambanaji wa haki za watu. Hakika! Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina,” amesema Zitto.

Haji anakuwa mbunge wa tatu kufariki dunia katika Bunge hili la 12 na ndani ya mwaka huu 2021.

Wengine waliotangulia ni; Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Martha Umbulla, aliyefariki tarehe 21 Januari 2021, Mumbai, nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu na Atashasta Nditiye wa Muhambwe mkoani Dodoma aliyefariki tarehe 12 Februari 2021, kwa ajili jijini Dodoma.

error: Content is protected !!