Wednesday , 27 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Zitto akwama Kisutu
Habari Mchanganyiko

Zitto akwama Kisutu

Zitto Kabwe
Spread the love

SHAHIDI wa Serikali kwenye kesi ya uchechezi inayomkabili Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo amekwamisha usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kutokana na dharura. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbele ya Huruma Shahidi, Hakimu Mkazi Mkuu kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo tarehe 29 Januari mwaka 2019 ambapo Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali, amedai shahidi amepata dharura.

Wakili Katuga ameieleza mahakama kuwa, walipanga kuwa na shahidi lakini kwa bahati mbaya amepata matatizo ya kifamilia, hivyo wanaomba ahirisho fupi.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Zitto, Jebrah Kambole aliiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi tarehe 27 Februari mwaka huu huku akidai kuwa mtuhumiwa alijipanga kusikiliza kesi hiyo licha ya kuwa anakabiliwa na majukumu mengine.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 27 Februari 2019.

Zitto alifikishwa Mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza, tarehe 2 Novemba 2018 kujibu mashtaka matatu ya uchochezi katika kesi ya jinai namba 327/2018.

Katika kesi ya msingi, Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Katika shitaka la kwanza, inadaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi alitoa maneno ya uchochezi.

Alitoa maneno ya uchochezi kuwa watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya cha Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua.

Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa ni maneno ambayo ni ya uchochezi yenye kuleta hisia za hofu na chuki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

error: Content is protected !!