Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto akabidhiwa mzigo wa Prof. Lipumba  
Habari za SiasaTangulizi

Zitto akabidhiwa mzigo wa Prof. Lipumba  

Spread the love

MAMBO yanzidi kwenda kombo ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo alikabidhiwa lundo la kadi na bendera ili amrejeshee Prof. Ibrahim Lipumba. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Katika mkutano uliofanyika jana tarehe 19 Machi 2019 Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, timu ya waliokuwa viongozi waandamizi wa CUF Bara na Visiwani walifika ofisini hapo na furushi la kadi na bendera na kisha kumwomba Zitto kumfikishia Prof. Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF-Taifa.

“Tunajua kuwa una uhusiano mzuri na Prof. Lipumba. Prof. Lipumba ni ndugu yako, mjomba wako na mzee wako, sasa tunakuomba hili furushi umfikishie yeye,” alisema Sheweji Mketo, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi CUF.

Baada ya Mketo kukabidhi mzigo huo, Babu Juma Duni Haji, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 akitokea CUF, alikabidhi kadi ya CUF kwa Zitto huku akisema “mrejeshee, atajua mwenyewe cha kufanya.”

Tuko la kurejeshwa kwa mzigo wa kadi hizo lilifanywa kabla ya Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF na timu yake kutoka Zanzibar na Bara kufika kwenye ofisi hizo kwa ajili ya utambulisho na kukabidhiwa kadi ya uanachama wa ACT-Wazalendo.

Maalim Seif alikwenda kwenye ofisi hizo ikiwa ni mara yake ya kwanza kabla na baada ya kuhamia ACT-Wazalendo. Mwanachama huyo mpya alikabidhiwa kadi namba moja ya chama hicho ambayo ilikuwa ikimilikiwa na mwanachama mwingine aliyeondoka kwenye chama hicho.

Kuhusu majengo ya CUF, Maalim Seif alisema kuwa, chama hicho kina majengo matatu akitaja kuwa yapo Mtendeni, Kilimahewa na Buguruni na kwamba ndiyo yanayomilikiwa na CUF.

“Kuna hayo majengo matatu ambayo ndiyo yanayomilikiwa na CUF, ofisi zingine wanachama ndio walikuwa wakijitolea. Sasa kama wanaona hakuna maana ya kubaki tena CUF na wakayachukua, hiyo ni wao.

“Kilichofanywa kwenye ofisi ya Mtendeni Zanzibar ni kuwa, wanachama walichukua vitu vyao na tumewaachia jengo lao. Kama jengo na makaratasi ndio chama, basi sisi tumewaachia lakini mimi naamini chama ni watu,” alisema Maalim Seif.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Tanesco yawasha mtambo namba 8 Bwawa Julius Nyerere

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!