Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto ajitosa sakata la DCI, DPP kufikishwa kortini kwa kushindwa kuchunguza wasiojulikana
Habari za Siasa

Zitto ajitosa sakata la DCI, DPP kufikishwa kortini kwa kushindwa kuchunguza wasiojulikana

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo
Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameahidi kutoa ushirikiano katika kesi ya jinai iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari Luqman Maloto, dhidi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), akiwatuhumu kushindwa kuchunguza matukio yaliyofanywa na watu wasiojulikana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo ya Jinai No. 5/2023, imefunguliwa kwenye Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam na imepangwa kuanza kusikilizwa mbele ya Jaji John Nkwabi, tarehe 8 Februari mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, leo tarehe 14 Januari 2023, Zitto ameandika akisema hatua ya Maloto kufungua kesi hiyo ni kubwa kwani imelenga kutafuta haki, hivyo atatoa ushirikiano kwa kueleza yote anayojua kuhusu matukio yaliyofanywa na watu wasiojulikana.

“Tofauti ya citizen na subject ndio hii. Asante sana sana ndugu @LuqmanMaloto
kwa hatua hii kubwa sana ya kutaka haki. Mimi binafsi nitakupa ushirikiano wote kwa yote ninayoyajua kuhusu watu kupotea, kuuwawa, kutekwa nk. Hii ndio maana ya never again. Urakoze chane chane,” ameandika Zitto.

Katika kesi hiyo ya jinai ambayo Maloto anawakilishwa na Wakili Hekima Mwasipu, mwanahabari huyo anaiomba mahakama itamke kwamba DCI na DPP wameshindwa kuwajibika vyema katika matukio yaliyofanywa na watu wasiojulikana kwenye nyakati tofauti.

Miongoni mwa matukio hayo ni la Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Chadema, Tundu Lissu, kushambuliwa na risasi Septemba 2017 akiwa jijini Dodoma. Kupotea kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL), Azory Gwanda na aliyekuwa kada wa Chadema, Ben Saanane.

1 Comment

  • ACT mtutetee na sisi wanyonge na hiri sakata ra mkaa kuzuiriwa na reseni za uvunaji za kusafirishia tunazo sheria eti zinapitiwa uku tumesimamishwa hii ni haki tufikisheni kirio chetu tunamikopo na mikataba ya boda boda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!