November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto aja na mikakati ya kuiteka Dar

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amewapa mbinu za ushindi viongozi wa majimbo wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwezi Oktoba 2019. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akifungua mkutano wake na viongozi hao uliofanyika leo tarehe 13 Julai 2019 jijini Dar es Salaam, Zitto amewataka kufanya utafiti katika maeneo yao, ili kujua changamoto zake kwa ajili ya kuandaa sera zitakazowavutia wananchi.

Zitto ameeleza kuwa, chama tawala cha CCM ambacho kimeshika dola, kimeshindwa kutatua kero sugu za jiji la Dar es Salaam, na kwamba udhaifu huo ni njia moja wapo ya kuipa ushindi ACT-Wazalendo katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Tunataka viongozi tujadiliane kwamba, mitaa yetu ina changamoto zipi, na sisi tuna sera zipi katika kutatua kero hizo. Na namna wananchi wataweza kuondoa changamoto zao,” amesema Zitto na kuongeza.

“Serikali ya CCM haijatoa majawabu ya kutatua changamoto hiyo. Kama tukitumia hoja hiyo wananchi wataona ACT ni chama cha kuwapa dhamana.”

Zitto amewaomba wanachama wa ACT-Wazalendo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuomba ridhaa ya chama hicho ya kugombea katika uchaguzi huo.

“Dar ina mitaa 561,tunahitaji wagombea 561, lakini zaidi ya hapo mitaa ina wajumbe wa kamati ya mtaa. Tunahitaji wagombea wa kamati za mtaa 5 mara 561.

“Tunahitaji kwenda kuhamasisha wanachama wetu waweze kwenda kuchukua majukumu ya uongozi, tuunde kamati za mitaa ili kutatua changamoto zilizopo,” amesema Zitto.

error: Content is protected !!