Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto afichua yaliyojificha ununuzi ndege mpya
Habari za SiasaTangulizi

Zitto afichua yaliyojificha ununuzi ndege mpya

Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini amefichua siri nzito iliyijifichika katika ununuzi wa ndege mpya ya Dreamliner 787-8. Anaripoti Mwandushi Wetu … (endelea).

Soma hapa chini kilichoandikwa na Zitto kuhusiania na ununuzi wa ndege hiyo.

Serikali inaficha jambo kuhusu Dreamliner 787-8, Tunaambiwa kwamba Ndege tunayonunua Boeing 787-8 Dreamliner Ndio kwanza inaundwa. Sio Kweli.

Ndege hiyo iliundwa mwaka 2009 na kinachofanyika Sasa ni kubadilisha Injini yake Kwa sababu Injini za ndege hizo zilikuwa na matatizo ya kuwaka moto ( imetokea Kwa Ethiopian na Nippon Air ya Japan ). Ndege iliyoundwa mwaka 2009 leo inafanyiwa marekebisho kidogo tunauziwa bei ya ndege mpya.!!

Hata hizi Bombardier tulizonunua hazikuundwa baada ya sisi kuweka order. Ndege hizi ziliundwa mwaka 2014 na zilikuwa tayari zimenunuliwa na Kampuni ya ndege ya Kazakhstan kabla ya baadaye kuuziwa sisi.

Ushahidi wa hili ni rahisi Sana, ukipanda ATCL Bombardier tafadhali soma maandishi madogo dirishani utaona S/N 0001519017-040 DATE 10/2014. Hiyo 10/2014 ni Oktoba, 2014.

Serikali inaficha jambo katika suala la ununuzi wa Ndege hii ya Dreamliner. Serikali inajua kuwa imenunua Terrible Teen Kwa bei kubwa kuliko ilivyostahili.

Shirika la ndege la Boeing linajua kuwa wametupiga bei ya kuruka na kutudanganyia Kwa kubadili injini. Serikali inajua kuwa haikusimamia maslahi ya Taifa katika mazungumzo kuhusu bei.

Hapakuwa na Government Negotiation Team Kama ilivyo kawaida ya manunuzi makubwa ya namna haya. (Bunge halikuhusishwa, baraza la mawaziri halikuhusishwa, wadau wa maendeleo hawakuhusishwa).

Bahati mbaya sana mazungumzo ya ununuzi wa ndege yalimhusisha Rais Magufuli na Katibu Mkuu Fedha James Doto peke yao (ambaye Lissu aliwahi kusema ni mtoto wa dada yake. Yani mtu na mjomba wake walijadiliana wakanunua ndege).

Shirika la Boeing wametumia uzoefu wetu mdogo kutupiga na Ni wajibu wa Watanzania wote Kwa kutumia mahusiano yetu yote duniani kuwataka Boeing wawajibike kwa udanganyifu wao kwetu.

Boeing wanapaswa kurudisha sehemu ya Fedha yetu. Ni aibu Kwa Kampuni kubwa Kama Boeing kuiibia Nchi masikini Kama Tanzania. Watanzania mnakumbuka sakata la Radar? Hii ni kurushwa zaidi ya radar. Hela zetu zirudi tujenge Reli au kuongeza Ndege.

Zitto Kabwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!