April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zimbabwe yatangaza mali za Mugabe

Marehemu Robert Mugabe enzi za uhai wake

Spread the love

SERIKALI ya Zimbabwe imeanika mali zilizoachwa na aliyekuwa rais wa taifa hilo, Robert Mugabe, aliyefariki dunia Septemba 2019. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gazeti la Serikali ya Zimbabwe, The Herald, Mugabe ameacha Dola za Marekani Milioni 10 (Tsh. 22.9 bilioni), nyumba nne mjini Harare, magari 10, mashamba na bustani.

Hata hivyo, gazeti hilo halijaorodhesha mali za Mugabe zilizoko nje ya nchi, pamoja na biashara aliyokuwa anafanya na mke wake, Grace Mugabe.

Katika hali isiyo ya kawaida, inadaiwa kwamba Mugabe hajaacha wosia kuhusu wamiliki wa mali zake.

Terrence Hussein, aliyekuwa Mwanasheria wa Mugabe amesema yeye pamoja na familia ya Mugabe, hawajapata wosia ulioachwa na kiongozi huyo wa Zimbabwe.

Lakini, kwa mujibu wa sheria za Zimbabwe, mali ikiwemo mashamba ya mtu aliyefariki pasina kuacha wosia, hugawanywa kwa mke au mweza na watoto wake.

error: Content is protected !!