KOCHA wa kikosi cha Real Madrid Zinedine Zidane amethibitisha kurejea kwa naohodha wa kikosi hiko Sergio Ramos kwenye mchezo wa leo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Mchezo huo wa mzunguko wa pili wa nusu fainali utachezwa kwenye Uwanja wa Stamford Brigde majira ya saa 4 usiku mara baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Ramos anarejea Uwanjani mara baada ya kukosekana kwenye mchezo uliopita kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya misuli ya mguu.
Kuelekea mchezo huo Zidane amesema kuwa nahodha na kiongozi wake anaerejea uwanjani kwenye mchezo wa leo na yupo tayari kucheza.
“Nahodha wetu na kiongozi amerejea na yupo na sisi, yupo tayari kucheza” alisema Zidane

Nahodha huyo mwenye miaka 35 ndio mchezaji mkongwe kwenye kikosi hiko kwa sasa ambaye amebeba mataji mengi ya Ligi Kuu na klabu bingwa barani Ulaya.
Kwenye mchezo wa leo Real Madrid inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya mabao kuanzia 2-2 na kuendelea ili iweze kufuzu kwenye hatua ya Fainali.
Chelsea wanaingia kwenye mchezo wa leo huku wakiwa na faida na matokeo ya mchezo wa kwanza wa bao 1-1, na hivyo kuwa na faida na bao la ugenini.
Kwenye mchezo wa leo Chelsea inahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kufuzu kwenye fainali ya michuano hiyo itakayochezwa Juni 28, 2021 jijini Instabul nchini uturuki.
Leave a comment