MAKOCHA Zinedine Zidane wa Real Madrid, Jurgen Klopp wa Liverpool na Hans Flick anaekinoa kikosi cha Bayern Munich wameteuliwa kati ya makocha watano walioingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya kocha bora wa dunia kwa mwaka 2020 zinatolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Tuzo hizo ambazo hutolewa kila mwaka na shirikisho hilo ambazo zinatambulika kwa jina la Tuzo za FIFA (FIFA Awards) ambazo zitatolewa tarehe 17 Desemba, 2020 katika vipengele tofauti.
Kuingizwa kwa makocha hao ni kutokana na mafaniko makubwa waliyoyapata kwenye msimu uliopita huku Hans Flick akiongoza Bayern Munich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) na Ligi Kuu nchini Ujerumani, mafanikio makubwa waliopata Klopp na Zidane ni kutwaa mataji ya Ligi Kuu nchini mwao.

Katika orodha hiyo pia wamejumuishwa kocha wa Leeds United inayoshiriki Ligi Kuu England, Marcelo Bielsa, sambamba na kocha mkuu wa Sevilla ya Hispania, Julien Lopetegul.
Leave a comment