Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Zidane aondoka Real Madrid
Michezo

Zidane aondoka Real Madrid

Zinedine Zidane
Spread the love

 

KOCHA wa klabu ya Real Madrid amechukua maamuzi ya kuachana na klabu hiyo mara baada ya kumaliza kwa msimu huu wa Ligi huku bila kuelezwa sababu iliyomfanya kuondoka klabuni hapo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umekuja ikiwa siku chache kabla ya msimu wa Ligi Kuu nchini Hispania kumalizika ambapo kocha huyo aliripotiwa na gazeti la Macca kutoka nchini Hispania kuwa ameshaongea na wachezaji wake na kuwaeleza uamuzi wake wa kuondoka mwishoni mwa msimu.

Zidane aliwambia maneno hayo wachezaji wake tarehe 8 Mei, 2021 siku moja kabla ya mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania dhidi ya Sevilla ambao ulimalizika kwa mabao 2-2.

Taarifa za kocha huyo kuondoka kwenye klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa miaka mitano katika vipindi tofauti zimekuja mara baada ya kuwambia wachezaji wake na watu wanaomzunguka kuwa anaondoka kwenye klabu hiyo.

Aidha taarifa kutoka nchini Hispania zimendelea kueleza kuwa kocha huyo amekutana na Rais wa klabu hiyo Florentino Perez na kumueleza uamnuzi wake wa kutaka kuondoka.

Taarifa rasmi ya kuondoka kwa kocha huyo huwenda ikatolewa katika muda mchache ujao na kueleza hatma yake kwa siku za mbeleni.

Wakati hayo yanaendelea tayari klabu hiyo ya Real Madrid imeshaanza mazungumzo ya kocha Massimiliano Allegri toka mwezi machi licha ya sasa kocha huyo kuwa kwenye mazungumzo na klabu za Juventus na Inter Milan ambayo imeamua kuachana na kocha wake Antonio Conte.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!