Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ziara ya Majaliwa Kagera yamng’oa afisa manunuzi
Habari za Siasa

Ziara ya Majaliwa Kagera yamng’oa afisa manunuzi

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Afisa Manunuzi wa Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera, Yesse Kaganda baada ya kutoridhishwa na viwango vya ubora wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe ambayo imejengwa kwa gharama ya Sh.2.5 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

“Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kila wakati anasisitiza usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa ili zitumike kwa ukamilifu na kujenga miradi yenye ubora, vigae hivi havijaanza kutumika tayari vimechakaa, afisa manunuzi huyu akae pembeni kwanza na vigae vipya viwekwe kwa gharama zake.”

Waziri Mkuu amesema Rais Samia ametoa fedha za kujenga na kukamilisha miradi ya maendeleo na kuhakikisha Serikali inasogeza huduma zote muhimu za kijamii lakini watendaji wachache wamekuwa wakishindwa kufuata maadili ya kazi zao na kujenga miradi isiyokuwa na ubora.

Ameyasema hayo jana Jumapili, tarehe 19 Septemba 2021, baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa Mikoa na Wilaya wahakikishe wanasimamia vyema matumizi ya fedha zilizotolewana Rais Samia katika kutekeleza miradi ya maendeleo na huduma za jamii ili kuleta tija na mabadiliko kwa wananchi.

“Malengo ya Rais wetu sasa yanaenda kutimia kwani anataka kila mwananchi apate huduma za afya hukohuko aliko, kuanzia ngazi ya kijiji tunajenga zahanati na baada ya kuwa zahanati za kutosha tunajenga kituo cha afya ambacho kina huduma zote muhimu, kama upimaji wa magonjwa yote, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto pamoja na wodi za wanaume na wanawake”. Alisema

Waziri Mkuu amewahakikishia wakazi wa Wilaya ya Karagwe kuwa ujenzi wa Hospitali hiyo utakamilika kwa wakati na kwa viwango kwani tayari fedha za kununua vifaa tiba vyote na mitambo ya mionzi zimetengwa.

Amesema wananchi pia wana wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutoa maoni kwani miradi hiyo inatekelezwa kwa kodi za wananchi. “Ninawaomba wananchi muendelee kuwa na imani na Serikali yenu pamoja na viongozi wake,”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!