Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ZEC yawaengua wagombea 15 Uwakilishi, 11 wa ACT-Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

ZEC yawaengua wagombea 15 Uwakilishi, 11 wa ACT-Wazalendo

Jaji Mkuu Mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid, Mwenyekiti wa ZEC
Spread the love

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewaengua wagombea 15 wa uwakilishi na saba wa udiwani, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukiuka masharti ya ujazaji fomu za uteuzi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Wagombea wa uwakilishi walioenguliwa 11 wanatoka Chama cha ACT-Wazalendo, mmoja kutoka Chama Cha Wananchi (CUF), Demokrasia Makini (1), UPDP (1) na mmoja kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi tarehe 19 Septemba 2020 na Thabit Idarous Faina Mkurugenzi wa Uchaguzi ZEC wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maamuzi ya rufaa za uteuzi wa wagombea wa uwakilishi na udiwani.

Faina amesema jana Ijumaa tarehe 18 Septemba 2020 ZEC ilifanya kikao cha kupitia mapingamizi 125 (mapingamizi kwa wagombea uwakilishi 84, na udiwani 41) pamoja na rufaa 64 kutoka kwa wagombea uwakilishi na 11 za wagombea wa udiwani.

Akitaja dosari zilizosababisha ZEC kuwaengua wagombea hao, Faina amesema baadhi yao hawakufuata kanuni za uchaguzi kwenye zoezi la ujazaji fomu, wagombea kudhaminiwa na watu waliodhamini wagombea wengine.

Makosa mengine ni baadhi ya wagombea ambao walikuwa watumishi wa umma kukiuka sheria za utumishi wa umma kugombea pasina kuomba ruhusa waajiriwa wao kwa mujibu wa sheria.

Faina amewataka wagombea waliofanikiwa kuteuliwa na ZEC kugombea kufuata sheria na kanuni za uchaguzi wakati wa kampeni ili kuepusha vitendo vya uvunjifu wa amani.

Wagombea uwakilishi wa ACT- Wazalendo walioenguliwa ni Haji Ali Haji (Tumbatu), Hassan Jani Masoud (Nungwi), Haji Makame(Kijini), Juma Duni Haji (Mtoni),Hasnie Abdallah Abeid (Bububu), Hamad Masoud Hamad (Ole), Omar Ali Shehe (Chakechake), Khamis Hassan Rashid (Chonga), Issa Said Juma (Micheweni), Isihaka Sharif (Wete).

Wagombea wa vyama vingine ni Juma Ally Juma mgombea wa Ole kupitia CUF, Abas Omar mgombea Jimbo la Ole (Demokrasia Makini), Yusuph Said Hamad, Mgombea Jimbo la Chakechake (UPDP) na Othman Khamis, Mgombea Jimbo la Mtambwe (CCM)

2 Comments

  • Hata ukiomba pasi ya kusafiri au kitambulisho cha uraia na ukikosea kujaza fomu unapewa nafasi ya kusahihisha . Iweje ni ZEC na NEC tu itoe uamuzi wa kipolisi namna hii? Imekuwa mtihani wa shule? DAH

  • Wanatunga sheria na kanuni mbovu, za kihuni na dhulma kisha wakishafanya uovu wao, wanadai kuwa wanatekeleza kwa mijibu wa sheria na kanuni. Sheria ambazo tangu mwanzo zilikuwa za hovyo kabisa. Hawa Tume na Serikali ya CCM wanatafuta kuitumbukiza nchi hii katika machafuko. CCM wanajua Zanzibar hawana lao, ila wanalazimisha tu kwa mabavu kushinda hizi chaguzi kwa kutumia Tume na vyombo vyengine vya usalama kama polisi, jeshi, na FFU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!