Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ZEC yamteua Maalim Seif kugombea urais
Habari za SiasaTangulizi

ZEC yamteua Maalim Seif kugombea urais

Spread the love

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imemteua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 27 na 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Maalim Seif alikuwa miongoni mwa wagombea 17 waliokuwa wamechukua fomu kuwania urais wa Zanzibar lakini jana Alhamisi tarehe 10 Septemba 2020 ilifanya uteuzi wa wagommbea 16 na Maalim Seif akiwekewa mapingamizi.

Mapingamizi hayo yaliwekwa na vyama vya DP na Demokrasia Makini wakidai fomu za Maalim Seif aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar zina kasoro.

 Soma zaidi:-

Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu mstaafu, Hamid Mahamoud Hamid amesema, baada ya kupitia mapingamizi hayo na utetezi wa Maalim Seif wameona hayana haja mashiko hivyo tume kumteua kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

Wagombea wengine 16 ni; Hussein Juma Salim (TLP), Issa Mohamed Zonga (SAU), Said Soud Said (AAFP), Said Issa Mohamed (Chadema), Khamis Fakhi Mgau (NRA) na Mfaume Hamis Hasaan (NLD).

Wengine ni; Dk. Hussein Mwinyi (CCM), Hamad Mohamed (UPDP), Shafii Hassan Suleiman (DP), Othuman Rashid Khamis (CCK), Ameir Hassan Ameir (Demokrasia Makini), Ali Omar Juma (Chaumma), Hamad Rashid (ADC), Juma Ali Khatib (Ada Thadea), Mussa Haji Kombo (CUF) na Mohamed Omar Shaame wa UMD.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!