Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ZEC: Uchaguzi mkuu Z’bar Oktoba 27 na 28
Habari za SiasaTangulizi

ZEC: Uchaguzi mkuu Z’bar Oktoba 27 na 28

Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu mstaafu, Hamid Mahmoud
Spread the love

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa urais na uwakilishi utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu mstaafu, Hamid Mahmoud wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 30 Julai 2020 visiwani humo.

Jaji Mahmoud amesema, kura ya mapema kwa watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi huo, itafanyika siku moja kabla yaani Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020.

“Natangaza rasmi tarehe ya uchaguzi itakuwa Jumatano tarehe 28 Oktoba mwaka huu, ndugu wananchi, sheria ya uchaguzi imetoa nafasi kufanyika kura ya mapema, napenda kuwajulisha, upigaji kura ya mapema itafanyika tarehe 27 oktoba 2020 siku moja kabla ya upigaji kura pamoja,” amesema Jaji Mahmoud.

Mwenyekiti huyo wa ZEC amesema, kura ya mapema itahusisha wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wa vituo vya uchaguzi na askari polisi watakaokuwa zamu siku ya uchaguzi. Wajumbe na watendaji wa tume.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura

“Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, upigaji kura mapema utahusisha watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi siku ya uchaguzi, watendaji hao ni wasimamizi wa uchaguzi, wasaidizi wasimamizi uchaguzi, wasimamizi wa vituo, askari polisi watakaokuwa kazini siku ya uchaguzi ,” amesema Jaji Mahmoud.

Siku hiyo ya uchaguzi mkuu, inafanana na ile iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

NEC ilisema shughuli ya uchukuaji fomu kwa wagombea ambapo wagombea wa ubunge na udiwani watachukua fomu tarehe 12 hadi 25 Agosti 2020, katika ofisi za NEC za halmashauri na kata nchi nzima.

Uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 25 Agosti 2020, huku kampeni zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!