January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Z’bar wahoji manufaa ya ziara za marais

Rais wa Marekani, Barrack Obama alipotembelea Tanzania

Spread the love

SERIKALI imebanwa ieleze Zanzibar inanufaikaje na misaada inayotolewa na marais wa matifa marafiki wanapotembelea Tanzania kama alivyofanya Rais Barack Obama wa Marekani. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Swali hilo limeulizwa bungeni leo mjini Dodoma na mbunge wa Viti Maalum, Amina Abdallah Amour (CUF).

Naye mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mery Mwanjelwa (CCM) akiuliza swali la nyongeza, ametaka kujua serikali inatoa kauli gani kwa Rais wa Burundi ambapo kwa sasa kuna vurugu na kusababisha wakimbizi wengi kuingia nchini.

Akijibu swali la nyongeza la Dk. Mwanjelwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema ni kweli wakimbizi wengi kutoka Burundi ambao wanafika nchini wamesababisha uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na uvamizi wa shule pamoja na uharibifu wa mazao.

Kwa mujibu wa Membe, Tanzania kama mdau wa amani watafanya kila linalowezekana kuhakikisha nchi hiyo haiingii katika machafuko.

Aidha, amewataka wananchi wa nchi ya Burundi kutulia huku viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wakiendelea kutatua mgogoro huo.

Mapema akijibu swali la msingi la Amour, Naibu wa wizara, Juma Mahadhi Juma, amesema kutokana na ziara ya Barck Obama, Tanzania imefanikiwa kupata vitabu 2.5 milioni vyenye thamani ya dola za Marekani milioni 5.5.

Alisema kupatikana kwa vitabu hivyo kumesaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi na kupunguza uwiano wa upatikani wa vitabu kwa wanafunzi.

error: Content is protected !!