Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Biashara Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro
BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the love

Kampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mara nyingine imeingia katika historia mpya kupandisha wageni wengi katika mlima Kilimanjaro.

Katika awamu hii wapanda mlima 228 wakiwemo mabalozi zaidi 11 wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wameshiriki kampeni ‘twende zetu kileleni’ ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika. Anaripoti Safina Sarwatt, Kilimanjaro …(endelea).

Akizumgumza baada hafla ya kuwaaga wapanda mlima 228 katika geti la Marangu, Mkurugenzi wa kampuni ya Zara tours adventures, Zainab Ansell amesema tangu kuanza kwa kampeni hiyo kumekuwepo na mwamko mkubwa kwa wageni na wenyeji kupanda mlima huo.

Amesema kampeni ya mwaka huu imekuwa ya aina yake kutokana na watu mashuhuri wakiwemo mabalozi zaidi 11 wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kushiriki.

“Kwakweli ni furaha kubwa sana kuona mwamko mkubwa kiasi hiki hadi mabalozi wetu wamekuja kupanda mlima ikiwa ni maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika, naamini kampeni hii itaendelea kuleta mwamko mkubwa wa watalii kuendelea kuja kupanda mlima Kilimanjaro,” amesema.

Amesema mwamko huo umetokana na juhudi ya Rais Samia Suluhu Hasan kupitia kampeni yake ya royal tours ambayo imeleta mabadiliko makubwa.

“Sisi wadau wa utalii tutaendele kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutoa huduma bora kwa wageni wanaokuja kwa ajili kutembea vivutio mbalimbali.

“Filamu ya Rais Samia imeleta matunda makubwa kwani watanzania wengi wameonesha mwamko kufanya utalii wa ndani na wameendelea kujitokeza na kupanda mlima Kilimanjaro,” amesema.

Amesema anajivunia kuwa na timu makini na vijana wanaojituma katika kufanya kazi kwa weledi.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini (TANAPA), Jenerali Mstaafu George Waitara

Mkuu wa wilaya Moshi, Kisare Makore amewapongeza mabalozi kujitoa kutangaza vivutio vya utalii nchini na kuwasisitiza kuendelea kutangaza utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro.

Amesema kupanda mlima siyo adhabu bali ni jambo la furaha hivyo wapande kwa lengo la kuutangaza mlima Kilimanjaro na kwa kufuata ushauri wataalam hususani waongozaji ili zoezi hilo lifanikiwa.

Katika hatua nyingine Makore ametoa wito kwa wananchi wanaoishi katika mwambao wa Pwani kuona wana wajibu wa kuhifadhi maeneo yao ili kuendeleza uwepo wa theluji katika Mlima Kilimanjaro.

Makori amesema Mlima Kilimanjaro unakabiliwa na changamoto za mabadikiko ya tabia nchi kutokana na  shughuli za kibinadamu ikiwamo ukataji wa miti usiozingatia kanuni za uhifadhi.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi nchini, Herman Batiho amesema washiriki hao wamepanda mlima kupitia mageti matatu yakiwemo geti la Lemosho, Machame na Marangu na wote watakutana katika kilele cha Mlima Kilimanjaro tarehe 9 Desemba 2023 huku wakipandasha Bendera ya Tanzania ambayo ndio siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Akizungumza kwa niaba ya mabalozi 11 wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali, Amidi wa muda wa mabalozi, Maadhi Maalimu amesema wajibu mkubwa  walionao ni kulinda na kutetea maslahi ya nchi na kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Mkurugenzi wa kampuni ya Zara tours adventures, Zainab Ansell

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini (TANAPA), Jenerali Mstaafu George Waitara amesema wameboresha huduma ndani ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikiwemo mawasiliano, vyoo, nyumba, pamoja na miundombinu ya barabara.

Jumla ya watu 228 wamepanda Mlima Kilimanjaro yakiwemo makundi mbalimbali kama vile taasisi za umma, taasisi binafsi, wasanii, mabalozi pamoja wanahabari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!