September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zanzibar imepumua – Rais Magufuli

Zanzibar

Spread the love

MIONGONI mwa mambo ambayo Rais John Magufuli anayojivunia katika uongozi wake wa miaka mitano, ni amani visiwani Zanzibar. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Amesema, Muungano kati ya Tanzania na Zanzibar umeendelea kuimarika licha ya kuwepo kwa tofauti ambazo zimeendelea kupatiwa ufumbuzi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Juni 2020, wakati akifunga Bunge la Jamhuri jijini Dodoma ili kutoa fursa ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

“Kama utakavyokumbuka moja wapao ya ahadi kubwa niliyoitoa ilikuwa ni kudumisha amani, umoja, mshikamano na mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Ninayo furaha kujulisha Bunge lako tukufu kwamba nimetimiza ahadi hiyo kwa vitendo, tumeendelea kubaki pamoja na kushirikiana licha ya tofauti zetu.

“Muungano wetu umeendelea kuimarika, tumeweza kushughulikia baadhi ya changamoto  ikiwemo suala la gharama ya kushusha mizigo, kufuta kodi ya ongezeko la thamani pamoja na malimbikizo ya kodi Sh 22.9 bilioni ambayo Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) liliyokuwa likidaiwa na Tanesco,” amesema. 

error: Content is protected !!