July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zambi: Naliona tatizo Vyama vya Ushirika

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa, haungi mkono viongozi wa kisiasa kushiriki katika Vyama vya Ushirika kwa maelezo ya kuwepo kwa uwezekano wa kuwepo kwa mitazamo tofauti. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Serikali pia imewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuhakikisha wanalipa posho kwa maofisa ushiriki wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati akijibu swali la Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua ni nini nafasi ya Ofisa Ushirika kama jicho la serikali katika kuhakikisha kuwa, Saccos zinatimiza malengo yake.

Natse pia alihoji ushiriki wa viongozi wa kisiasa kwenye Saccos ambao umekuwa ni tatizo kubwa.

“Majukumu ya Ofisa Ushirika yameainishwa katika maendeleo ya ushirika nchini katika Sera ya Maendeleo ya mwaka 2002 na sheria namba 6 ya mwaka 2003 ya Vyama vya Ushirika,” amesema Zambi.

Alitaja majukumu hayo ni kukagua na kusimamia Vyama vya Ushirika, kutoa elimu kuhusu ushirika, majukumu ya vyama vya ushirika, kubainisha kuhusu malalamiko na vyama vya ushirika na kutafuta ufumbuzi.

“Katika kukabiliana na changamoto za kuimarisha usimamizi wa uendeshaji wa vyama vya ushirika, Serikali imeunda Tume ya Maendeleo ya Ushirika na kuipa mamlaka ya kusimamia moja kwa moja majukumu ya maafisa ushirika kuanzia ngazo ya taifa hadi wilaya,” amesema.

Ametaja sheria namba 6 ya mwaka 2013 ya vyama vya ushirika ambayo imeanza kutumika rasmi Januari mwaka 2014 ambayo imeainisha mambo mbalimbali ikiwemo kuwazuia viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma.

error: Content is protected !!