September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zakaria Hanspope afariki dunia

Zacharia HansPope

Spread the love

 

ZAKARIA Hanspope, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara 2020/21, Simba ya Dar es Salaam, amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hanspope amefikwa na mauti usiku wa Ijumaa tarehe 10 Septemba 2021, katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam humo alipokuwa akipatiwa matibabu.

Simba kupitia kurasa zake za kijamii, imeweka picha ya Hanspope ambaye pia ni mfanyabiashara akiwa ameshika kombe la Azam Sports Federation Cup waliloshika dhidi ya watani zao Yanga mkoani Kigoma.

Picha hiyo imeambatana na maneno “Uongozi wa Klabu ya Simba umepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Zacharia HansPope ambaye amefariki dunia usiku huu.”

Simba imesema taarifa zaidi zitawajia kupitia kurasa zao.

error: Content is protected !!