
Spread the love
KIMBUNGA cha Irma kimesababisha vifo vitatu baada ya kutua katika jimbo la Florida kikitokea kisiwa cha Marco magharibi mwa pwani ya Florida nchini Marekani, anaandika Irene Emmanuel.
Kimbunga hicho kilichosababisha uharibifu mkubwa kina kasi ya kilomita 192 kwa saa lakini kwa sasa kimeshuka kutoka kiwango cha tatu hadi cha pili.
Zaidi nyumba milioni 3.4 katika jimbo hilo hazina nguvu za umeme kufuatiwa na kimbunga cha Irma kilichoanza jana na sehemu za mji wa Miami zimefurika maji kutokana na kimbunga hicho.
More Stories
Milioni 91 wapona corona duniani
Papa Francis atembelea Iraq
Kesi mauaji ya Jamal Khashoggi yaanza tena