January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zaidi ya 30 wapoteza maisha katika ajali Singida

Spread the love

Watu zaidi ya 30 wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kupata ajali. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Akizungumza kwasimu kutoka eneo la ajali Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ila kwa kuwa alikuwa kwenye eneo la uokoaji na miili ilikuwa bado inaopolewa hakuweza kutaja idadi halisi akiahidi kutoa idadi hiyo baadaye.

Basi lililopata ajali limeripotiwa kuwa ni Taqbir linalofanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo hilo la kijiji cha Kizonzo, kilometa chache nje ya mji wa Shelui,walisema kuwa basi hilo lilipata ajali baada ya kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.

Taarifa zaidi zitawajia baadaye…….

error: Content is protected !!