February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zahera, Amri Said washinda Tuzo Ligi Kuu

Spread the love

MAKOCHA Mwinyi Zahera wa klabu ya Yanga na Amri Said wa Mbao kutoka jijini Mwanza wameshinda tuzo za kocha bora wa mwezi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 ambazo zimeanza kutolewa rasmi msimu huu na Shirikisho la Mpiwa wa Miguu Tanzania (TFF). Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Tuzo ya kocha bora wa mwezi Septemba imeenda kwa Mwinyi Zahera ambaye mpaka sasa ameiongoza Yanga kwenye michezo mitano ya Ligi Kuu na kufanikiwa kushinda mechi nne na kwenda sare mchezo mmoja na kujikusanyia jumla ya pointi 13 na kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu.

Kwa upande wa Amri Said ambaye ameshinda tuzo ya kocha bora mwezi Agosti mpaka sasa amepoteza mchezo mmoja tu baada ya kuiongoza Mbao FC kwenye michezo nane ya Ligi Kuu na kujikusanyia jumla ya pointi 14 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Tuzo hiyo ya kocha bora wa mwezi imeanzishwa kwa mara ya kwanza na kamati ya tuzo za wachezaji wa Ligi Kuu Bara kwa lengo la kutambua mchango wa kocha husika katika ligi hiyo.

error: Content is protected !!