October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yondani avuliwa unahodha Yanga, Ajibu achukua nafasi

Spread the love

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amemvua unahodha, Kelvin Yondani kutokana na mchezaji huyo kutofika mazoezini bila taarifa yoyote, nafasi yake kuchukuliwa na  Ibrahim Ajibu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, imeeleza kikosi cha wachezaji wasioenda kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kuendelea na mazoezi pamoja na kuondolewa kwa Yondani katika nafasi hiyo.

“Wachezaji waliobaki Dar es Salaam, wanaendelea na mazoezi leo katika viwanja vya polisi ufundi kurasini jijini Dar es Salaam baada ya mapumziko ya siku nne kwa baadhi ya wachezaji ambao hawakusafiri na timu visiwani Zanzibar kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi.” Ilienda sehemu ya taarifa hiyo.

Siyo mara ya kwanza kocha huyo kuchukua maamuzi magumu kwa baadhi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho kutokana kuhitaji usawa na nidhamu kwa wachezaji wote ndani ya klabu hiyo kiasi cha hivi karibuni kumuondoa katika kikosi kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya baada ya kuondoka kambini bila taarifa kwa kushinikiza alipwe madai yake.

Mazoezi hayo yaliongozwa na kocha huyo yalikuwa ya utimamu wa mwili pia kwa upande wa uwanjani kulikuwa na mafunzo maalumu juu ya umakni uwanjani (Concentration) pamoja na umaliziaji kwenye safu ya ushambuliaji.

error: Content is protected !!