Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima
Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Mkurugenzi Mkuu wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo
Spread the love

 

WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo ili kuwanusuru wananchi wake na baa la njaa, kampuni ya mbolea -Yara imezindua bima ya mazao ili kuwakinga wakulima dhidi ya hasara mbalimbali kwenye sekta hiyo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika uzinduzi wa bima hiyo leo tarehe 28 Machi 2022, Mkurugenzi wa Yara Tanzania, Winstone Odhiambo amesema Yara kupitia mpango wake wa Africonnect inashirikiana na kampuni ya bima ya Jubilee Insurance kukata bima hizo.

Amesema kuwa awali mpango wa Africaconnect ilizinduliwa mwaka 2022 ambapo wakulima wa mpunga 83,000 waliojiunga na mpango huo wananufaika na huduma za kifedha, upatikanaji wa mbolea bora, huduma za ugani pamoja soko la uhakika kwa mazao yao.

“Hatua hii ni kubwa kwetu tunaposhughulika kuwawezesha wakulima kupata riziki yao na kulinda usalama wa chakula. Kwa kujiunga na Africaconnect, kampuni ya Jubilee Insurance imeongeza msukumo wa kufanya kilimo Tanzania kuwa thabiti na chenye faida” amesema Odhiambo.

Mbali na Jubilee washirika wengine wa Africaconnect ni benki ya Equity, Corteva Agriscience, Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na Uendeshaji Mbegu za Kilimo (Agriculture Seed Agency) na kampuni ya Murzah Wilmar Rice Miller Ltd.

Odhiambo amesema wakulima wanaopenda kujiunga na mpango huo wafike kwa mawakala wa mbolea wa Yara walio karibu nao, tawi lolote la Benki ya Equity au wapige simu bure kwenda namba 0800750188.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Jubilee Insurance, Dipankar Acharya amesema mpango huo utawalinda na kuwanufaisha wakulima dhidi ya hasara ya mazao.

“Tumefurahi kuwa washirika wa Africaconnect ili kuwalinda wakulima na hasara za mazao zinazosababishwa na majanga ya asili kwa kuwapa bima ya mazao na ushughulikiaji bora wa hatari wanazokabiliana nazo katika kilimo. Kwa kuwepo mpango huu wa bima ya mazao, sasa tunatarajia wakulima watalima kwa matumaini makubwa,” amesema.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Equity Bank, Isabela Maganga amesema Benki ya Equity kwa mwaka 2022 ilitoa mikopo yenye thamani ya Sh1.1 bilioni kwa wakulima 1,400 wa mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Arusha, Manyara na Iringa kupitia mpango wa Africaconnect.

Amesema asilimia 30 ya mikopo yote itolewayo na benki ya Equity, huwalenga wakulima nchini.

Wakati, Meneja wa Yara Digital Solution kwa nchi ya Tanzania na Rwanda, Deodath Mtei amesema wataendelea kuwashika mikono wakulima kwa kuhakikisha kuwa wanazidi kupata ujuzi wa kulima kisasa ili wapate faidi maradufu.

Upendo Daniel, mjane anayejishughulisha na kilimo cha mpunga wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro amesema kuwa kupitia mpango wa Africannect amefanikiwa kuongeza uzalishaji katika shamba lake la robo heka kutoka magunia manne hadi 11 ya kilo 100.

1 Comment

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAISI KULE ULIKOENDA KUONA)…

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!