MWENYEKITI wa Yanga, Dk. Mshindo Msolwa leo amezindua kampeni ya kuelekea mfumo wa mabadiliko ya kiuendeshaji ambayo yatakuwa chini ya kamati ndogo ya mabadiliko ya kimfumo itakayosimamiwa na Mwanasheria Alex Mgongolwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mabadiliko hayo ambayo yanafadhiliwa na kampuni ya GSM yataifanya klabu hiyo kujiendesha katika mfumo wa kisasa ambao utakuwa unakalibisha wawekezaji na kufanya klabu hiyo kujitemea na kukua kiuchumi.
Katika zoezi hilo Mwenyekiti Msolwa ameleeza kuwa moja ya lengo lake kama kiongozi ni kubadilisha muundo wa klabu hiyo ili iweze kuingia kwenye mfumo wa kisasa tofauti na waliouzoea.
“Moja ya dhamila yangu nilivyokuwa naingia kwenye uongozi ilikuwa ni swala la kubadilisha muundo wa uendeshaji wa klabu na sasa ndoto inakalibia kutimia,” alisema Msolwa.
Awali Yanga ilimleta Carraca Antonio Domingo mtaalamu wa uendeshaji wa soka la kisasa kutoka klabu ya Benifica ya Ureno ilikuja kuwapa uzoezi katika maswala hayo ambayo kwa sasa mchakato wake unaelekea kuanza.
Yanga itakuwa klabu ya pili kuingia katika mfumo wa mabadiliko nchini baada ya watani wao klabu ya Simba kufanya hivyo kwa kutumia mfumo wa hisa ambao ambao wanachama wanaumiliki wa asilimia 51, na Mohamed Dewji ‘MO’ ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi anamili asilimia 49.
Leave a comment