Saturday , 9 December 2023
Home Kitengo Michezo Yanga yazidi kuikaribia Simba, bado tatu
Michezo

Yanga yazidi kuikaribia Simba, bado tatu

Ibrahim Ajibu, mshambuliaji wa Yanga
Spread the love

YANGA imerudi nafasi ya pili baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hiyo ni kutokana na kufikisha pointi 43 baada ya kucheza mechi 20, sasa ikizidiwa pointi tatu tu na vinara, Simba SC.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na Shomari Lawi kutoka Kigoma, aliyesaidiwa na Charles Simon wa Dodoma na Agnes Pantaleo wa Arusha, mabao ya Yanga yalifungwa na Ibrahim Ajib, Yussuph Mhilu na Juma Shemvuni aliyejifunga.

Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza timu hizo zikimaliza bila kufungana, mvua ya mabao ikaanza kuwamiminikia Kagera Sugar kipindi cha pili.

Alianza mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Ibrahim Ajib dakika ya 53 kufunga kwa penalti baada ya beki Mzanzibari wa Kagera Sugar, Adeymum Saleh Ahmed kuunawa mpira kwenye eneo boksi.

Akafuatia winga Yussuph Mhilu kufunga la pili dakika ya 75 akimalizia majaro iliyoingizwa kwenye lango la Kagera na kiungo mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa.

Zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika, beki wa Kagera Sugar Juma Shemvuni akamfunga kipa wake, Ramadhani Chalamanda katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na kiungo wa Yanga, Yusuph Mhilu aliyetokea benchi cha pili.

Katika mchezo wa leo, kiungo Mzimbabwe Thabani Scara Kamusoko alicheza kwa dakika 71 baada ya kukosekana uwanjani tangu Septemba 16, mwaka jana alipoumia kwenye mechi dhidi ya Maji Maji mjini Songea.

Mabingwa hao wa Tanzania watarudi uwanjani Jumatatu kumenyana na Stand United Uwanja wa Taifa, kabla ya kusafiri kwenda Botswana kwa mchezo wa marudiano na Township Rollers Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako wanatakiwa kushinda 2-0 waingie hatua ya makundi, baada ya kufungwa 2-1 Jumanne Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wenzako wameshakuwa mamilionea hapa wewe unasubiri nini?

Spread the love  WIKIENDI imefika na ukiachana na mvua za Dar es...

Michezo

Manchester City vichwa chini Ligi Kuu England

Spread the love MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Uingereza klabu yaManchester City...

Michezo

Piga mkwanja wa kutosha katika usiku wa kibabe kati ya Man United vs Chelsea

Spread the love USIKU wa leo katika dimba la Old Trafford utapigwa mchezowa...

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

error: Content is protected !!