March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yawaondoa wanne kikosini

Spread the love

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewaondoa kikosini wachezaji Haji Mwinyi, Ramdhani Kabwili, Pius Buswita na Said Makapu kutokana na sababu za utovu wa nidhamu waliouonyesha wakati wa mazoezi ya timu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Sababu za kabwili kuondolewa kwenye kikosi ni baada ya kuchelewa wakati wa kula timu ilipokuwa kambini, huku kwa upande wa wengine watatu walitakiwa kuwapo uwanjani wakati timu hiyo ilipokuwa ikiminyana na Stand united licha ya kutokuwa sehemu ya kikosi katika mchezo huo lakini waliamua kukaidi na kuingia mitini. 

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten amesema kocha huyo ameamua kuchukua maamuzi hayo na kutokana na utovu wa nidhamu waliouonesha wachezaji hao na hawatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Coastal Union.

“Mwalimu aliwaondoa kikosini kwa sababu za kinidhamu na adhabu yao itaendelea mpaka baada ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu na baadae swala lao litarudishwa kwa uongozi ili kuweza kujadiliwa na kuona nini kinaweza kikafanyika na hatua zaidi kuchukuliwa,” amesema Dismas Ten.

Aidha msemaji huyo aliongezea ya kuwa adhabu hizo ni za ndani ambazo hawawezi kuziweka hadhalani lakini mashabiki wanapaswa kujua kwa sasa wachezaji hao hawapo kambini pamoja na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya michezo ijayo ya ligi.

error: Content is protected !!